Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w15 4/15 uku. 32
  • Je, Mti Uliokatwa Unaweza Kuchipuka Tena?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Mti Uliokatwa Unaweza Kuchipuka Tena?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Ayubu Alikuwa na Uhakika Kwamba Kungekuwa na Ufufuo
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Mzeituni Unaostawi Katika Nyumba ya Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • ‘Lo! Jinsi Kilivyo Kina cha Hekima ya Mungu!’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Mzeituni Wenye Kuzaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
w15 4/15 uku. 32
Mti uliokatwa ukichipuka tena

Je, Mti Uliokatwa Unaweza Kuchipuka Tena?

HUENDA mzeituni ukaonekana hauvutii sana unapolinganishwa na mwerezi maridadi wa Lebanoni. Hata hivyo, mzeituni una uwezo wenye kustaajabisha sana wa kuhimili hali ngumu. Inakadiriwa kwamba mizeituni fulani imekuwapo kwa miaka 1,000 hivi. Mizizi ya mzeituni ni mirefu sana hivi kwamba inaweza kuusadia mti huo kukua tena hata kama shina la mti huo limekufa. Ikiwa mizizi hiyo iko hai, basi mti huo utachipuka tena.

Mwanaume mwaminifu Ayubu alikuwa na uhakika kwamba hata kama angekufa, angeishi tena. (Ayu. 14:13-15) Alitumia mfano wa mti, labda ule wa mzeituni, ili kuonyesha uwezo wa Mungu wa kumfufua. “Kwa maana hata kwa ajili ya mti kuna tumaini,” akasema Ayubu. “Ukikatwa, utachipuka tena.” Mvua inaponyesha baada ya ukame mkali, mabaki ya mzeituni ulionyauka kabisa yanaweza kuchipuka tena kutoka kwenye mizizi yake na kutokeza ‘matawi kama mmea mpya.’—Ayu. 14:7-9.

Kama vile mkulima anavyotamani kuona mizizi ya mzeituni uliokatwa ikichipuka tena, Yehova Mungu anatamani sana kuwarudisha kwenye uhai watumishi wake waliokufa na watu wengine wengi. (Mt. 22:31, 32; Yoh. 5:28, 29; Mdo. 24:15) Itakuwa shangwe iliyoje kuwakaribisha wale watakaofufuliwa na kuwaona wakifurahia tena uhai!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki