Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w15 10/15 uku. 3
  • ‘Endeleeni Kuwaheshimu Sana Watu wa Namna Hiyo’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Endeleeni Kuwaheshimu Sana Watu wa Namna Hiyo’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova Ni Nini?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
  • Jinsi Ambavyo Baraza Linaloongoza Limepangwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Kushirikiana na Baraza Linaloongoza Leo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Mabadiliko Katika Baraza Inayoongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
w15 10/15 uku. 3
Mwonekano wa mkutano wa Halmashauri ya Baraza Linaloongoza

‘Endeleeni Kuwaheshimu Sana Watu wa Namna Hiyo’

TANGU mwaka wa 1992, Baraza Linaloongoza limewaweka rasmi wazee wakomavu na wenye uzoefu ili wasaidie kazi katika halmashauri zake mbalimbali.a Wasaidizi hao, ambao ni miongoni mwa “kondoo wengine,” wanalisaidia sana Baraza Linaloongoza. (Yoh. 10:16) Wanahudhuria mikutano ya kila juma ya halmashauri wanazotumikia, nao hutoa maelezo na mapendekezo yao. Baraza Linaloongoza ndilo hufanya uamuzi wa mwisho, lakini wasaidizi wao hutekeleza maamuzi hayo na kutimiza mgawo wowote wanaopewa. Pia, wao huandamana na washiriki wa Baraza Linaloongoza kwenye makusanyiko ya eneo ya pekee na ya kimataifa. Isitoshe, wanaweza kupewa mgawo wa kutembelea ofisi za tawi wakiwa wawakilishi wa makao makuu.

Msaidizi mmoja ambaye ametumikia tangu mpango huu ulipoanzishwa, anasema hivi: “Ninapotimiza migawo yangu, ninalisaidia Baraza Linaloongoza kutimiza kikamili majukumu yake.” Ndugu mwingine aliyetumikia kwa miaka 20 akiwa msaidizi, anasema hivi: “Imekuwa heshima kubwa sana kwangu na sikuwahi kutarajia jambo hilo.”

Baraza Linaloongoza limewakabidhi wasaidizi wake majukumu mengi na linathamini kazi bora inayofanywa na ndugu hao washikamanifu na wenye bidii. Acheni sote ‘tuendelee kuwaheshimu sana watu wa namna hiyo.’—Flp. 2:29.

a Tazama sanduku lenye kichwa “Jinsi Baraza Linaloongoza Linavyoshughulikia Mambo ya Ufalme” katika sura ya 12 ya kitabu Ufalme wa Mungu Unatawala! ili kupata muhtasari wa majukumu ya halmashauri sita za Baraza Linaloongoza.

Wasaidizi wa Halmashauri za Baraza Linaloongoza

Halmashauri ya Waratibu

  • John Ekrann

  • Robert Wallen

Halmashauri ya Wafanyakazi

  • Gerald Grizzle

  • Patrick LaFranca

  • Daniel Molchan

  • Ralph Walls

Halmashauri ya Uchapishaji

  • Don Adams

  • Robert Butler

  • Harold Corkern

  • Donald Gordon

  • Robert Luccioni

  • Alex Reinmueller

  • David Sinclair

Halmashauri ya Utumishi

  • Gary Breaux

  • Joel Dellinger

  • Seth Hyatt

  • Christopher Mavor

  • Baltasar Perla, Jr.

  • William Turner, Jr.

  • Robert Wallen

  • Leon Weaver, Jr.

Halmashauri ya Ufundishaji

  • Ronald Curzan

  • Kenneth Flodin

  • William Malenfant

  • Mark Noumair

  • David Schafer

Halmashauri ya Uandikaji

  • Robert Ciranko

  • James Mantz

  • Izak Marais

  • Gene Smalley

  • John Wischuk

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki