Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 9/90 uku. 1
  • Mheshimu Muumba wa Vitu Vyote

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mheshimu Muumba wa Vitu Vyote
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • TOA USHAHIDI WENYE MAFANIKIO
  • SHULENI
  • Mageuzi Yajaribiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Kutangaza Habari Njema—Kwa Kitabu Creation
    Huduma Yetu ya Ufalme—1988
  • Je, Mungu Alitumia Mageuzi Kuumba Uhai?
    Amkeni!—2006
  • Je, Fundisho la Mageuzi Linapatana na Biblia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1990
km 9/90 uku. 1

Mheshimu Muumba wa Vitu Vyote

1 Wakati wa karne ya 19, Shetani alitokeza mpango wa hila ili kupofusha ainabinadamu—ile nadharia ya mageuzi. (2 Kor. 4:4) Nadharia hii ni ukanushaji wenye ufidhuli wa simulizi la Biblia la uumbaji na kuanguka kwa binadamu katika dhambi. Ingefanya ukombozi wa Yesu na fundisho la Biblia juu ya Ufalme na uhai wa milele kuwa yasiyo na maana. Zaidi ya hilo, nadharia ya mageuzi hutayarishia njia jeuri na vita, ukosefu wa adili kingono, na namna zote za uasi-sheria. Ni nani ataonya ainabinadamu juu ya hatari za fundisho hili lenye kuleta kifo?

2 Wakati wa mwezi Septemba, tutakuwa tukifanya hivyo, kwa kuwa tutakuwa na shughuli tukipiga mbiu kwamba Yehova ndiye Muumba. Katika huduma ya nyumba kwa nyumba, pindi za kupumzika katika kazi ya kimwili, na shuleni, tutakuwa tukionyesha watu kitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? Twatamani kila mtu ajue jinsi nadharia ya mageuzi humvunjia heshima Muumba wa ainabinadamu.

TOA USHAHIDI WENYE MAFANIKIO

3 Unapotoa ushahidi vivi hivi au nyumba kwa nyumba, huenda ukataka kuanza mazungumzo kwa kurejezea habari zinazotolewa pindi kwa pindi kuhusu maoni imara yanayoshikiliwa na baadhi ya watu juu ya mageuzi. Semi nyingi zimetolewa kuhusu swala la kama nadharia ya mageuzi yapasa kufundishwa katika shule za umma. Ingawa huenda mtu akawa amesoma au kusikia mengi juu ya hoja na majadiliano motomoto kuhusu habari hii, bila shaka ataiona kuwa ya kupendeza taarifa iliyo rahisi kueleweka katika Biblia inayohusu habari hii moja kwa moja. Halafu rejezea yale yanayotaarifiwa kwenye Waebrania 3:4. Soma andiko na kulieleza kifupi.

4 Mtu huyo akionekana kuwa na mbetuko wa kidini, ungeweza kutaja kwamba mara nyingi watu wa kidini pamoja na wale wanaoamini mageuzi wanaihesabia “Asili” isiyo na utu au “Asili Mama” yenye utu kuwa ndiyo kani yenye kuumba vitu vyote vizuri ajabu tuvionavyo kutuzunguka. Lakini Biblia haimwachi bila utambulisho Mfadhili wetu Mtukufu na Muumba wa huu ulimwengu wote mzima wenye kustaajabisha. Fikira zaweza kuvutwa kwenye Ufunuo 4:11. Baada ya kusoma andiko, huenda mtu huyo akataka kujieleza kuhusu jambo hilo. Waweza kuunganisha mazungumzo na jambo moja au mawili kutoka kitabu Creation na, ikifaa, umtie moyo akisome.

SHULENI

5 Muhula mpya wa shule uanzapo, nyinyi nyote watumishi wachanga wa Yehova mtataka kupitia kitabu chenu cha Creation na kufikiria njia mbalimbali za kuwafanya wanafunzi wenzenu pamoja na walimu wapendezwe nacho. Baadhi yenu wameona kwamba kukiacha tu kichapo hicho juu ya dawati huvuta mazungumzo. Wengine wamewaendea walimu na wasimamizi wa shule kwa habari ya uumbaji na wameweza kugawanya vitabu kadhaa kwa njia hiyo.

6 Sisi sote hushangilia taraja la kuishi katika ulimwengu ambamo kila mmoja atamheshimu Yehova. Katika Ufunuo, Yohana aliona viumbe-roho wenye uzuri wa ajabu wakisujudu mbele za Yehova na kupiga mbiu, “Umestahili wewe, Bwana [Yehova, NW] wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.” (Ufu. 4:11) Sisi na turudishe mwangwi wa maneno hayo katika huduma yetu wakati wa Septemba!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki