Anwani za Ofisi za Tawi
◼ Tafadhali mfahamu kwamba kila mwaka orodha ya karibuni zaidi ya ofisi za Mashahidi wa Yehova kuzunguka ulimwengu huandaliwa nyuma ya Kitabu-Mwaka. Orodha hiyo ni ya kuwarahisishia mambo na ya kutumiwa nanyi. Mnaweza kuokoa wakati na pesa kwa kurejezea Kitabu-Mwaka cha karibuni zaidi badala ya kupiga simu au kuandika barua ili mpate anwani za ofisi za tawi katika nchi nyinginezo.