Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/96 uku. 1
  • Kuitangaza Habari Njema ya Jambo Lililo Bora

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuitangaza Habari Njema ya Jambo Lililo Bora
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kutangaza Habari Njema-Kwa Magazeti
    Huduma Yetu ya Ufalme—1989
  • Mnara wa Mlinzi na Amkeni!—Majarida ya Wakati Ufaao Yenye Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Kutumia Vema Mnara wa Mlinzi na Amkeni!
    Huduma Yetu ya Ufalme—1993
  • Magazeti Yatangaza Ufalme
    Huduma Yetu ya Ufalme—1998
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 10/96 uku. 1

Kuitangaza Habari Njema ya Jambo Lililo Bora

1 Kwa miaka 117 Mnara wa Mlinzi limetumika likiwa mteteaji wa kweli ya Biblia. Kwa sasa, nakala 18,950,000 za kila toleo zinachapwa katika lugha 125. Amkeni! pia limetetea Neno la Mungu kwa muda mrefu, na sasa nakala zalo 15,730,000 hugawanywa katika lugha 80.—Linganisha Wakolosai 1:23.

2 Magazeti Hutosheleza Uhitaji wa Kiroho: Mnara wa Mlinzi na Amkeni! yamenufaisha mamilioni ya watu wenye mioyo ya haki kwa kusaidia kutosheleza uhitaji wao wa kiroho. Makala zenye kujenga imani zinatangazwa. Kwa kielelezo, katika Mnara wa Mlinzi la Februari 1, 1996, tulijifunza habari iliyoshughulikia uhitaji wa kumtumaini Yehova na Neno lake. Toleo la Mnara wa Mlinzi, la Machi 1, 1996, lilitutia moyo tuendelee kuwa wenye shughuli katika utumishi wa Yehova na kufuliza kumtarajia. Yale mazungumzo yaliyotia ndani mambo mengi juu ya unabii wa Sefania yalisisimua kama nini! Kisha kulikuwa na yale mazungumzo yenye kuimarisha imani juu ya uaminifu-mshikamanifu wa Kikristo katika Mnara wa Mlinzi la Machi 15, 1996. Toleo la Mei 15, 1996, lilikazia thamani ya kusoma na kujifunza Neno la Mungu kwa ukawaida. Makala hizo zimesaidia kuongeza kina cha uelewevu wetu wa Neno la Mungu, na uthamini wetu kwa ajili ya Ufalme wake umeongezwa.

3 Zaidi ya hayo, magazeti hayo yana makala zenye kutumika, za wakati ufaao, juu ya mwenendo wa kimungu, maadili ya Kikristo, na habari nyinginezo zenye maana sana. Zinashughulikia kwa uzito masuala halisi yanayoathiri maisha yetu. Likiwa tokeo, twafurahia hali ya maisha yenye ubora zaidi tungojapo utimizo wa ahadi za Mungu wa jambo lililo bora hata zaidi katika wakati ujao.—Isa. 48:17; 1 Tim. 6:19.

4 Pitio fupi la yale yanayotaarifiwa kwenye ukurasa wa 4 wa kila toleo la Amkeni! hutupa sisi sababu nzuri ya kupendekeza gazeti hili kuwa habari bora zaidi ya kusomwa na watu kila mahali, vijana kwa wazee vilevile. Hapo lataarifu hivi: “Amkeni! ni gazeti la kupatia familia nzima nuru. Huonyesha jinsi ya kukabiliana na matatizo ya wakati wetu. Huripoti habari, husimulia juu ya watu katika nchi nyingi, huchunguza dini na sayansi. Lakini si hayo tu. Huchunguza sana matukio ya sasa na hutoa maana ya kweli ya matukio hayo, hata hivyo linabaki sikuzote bila kuingilia siasa wala kutukuza jamii moja ya watu juu ya nyingine. La maana kuliko yote, gazeti hili hujenga uhakika katika ahadi ya Muumba ya kuleta ulimwengu mpya wenye amani na usalama ambao uko karibu kuchukua mahali pa mfumo wa mambo uliopo mwovu na usiotii sheria.”

5 Shiriki Magazeti na Wengine: Uwe mwenye ukarimu katika kugawanya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! (Linganisha 1 Timotheo 6:18.) Uwe na nakala kadhaa ili uweze kuzitoa kwa mtu yeyote yule ambaye huenda ukakutana naye. (Mhu. 11:6) Sisi sote, kutia ndani watangazaji vijana na wapya, twaweza kushiriki kikamili katika kugawanya magazeti mwezi huu kwa kutumia utoaji mfupi mbalimbali unaotegemea makala za wakati ufaao zilizomo katika matoleo ya sasa. Pata kufahamu vizuri yaliyomo, na kuyatoa kwa moyo mweupe na ukiwa na usadikisho.

6 Mnara wa Mlinzi na Amkeni! yana habari ambayo kila mtu ahitaji. Kuyagawanya ni mojapo njia bora zaidi tuwezayo kusaidia wengine wajifunze habari njema kwamba jambo lililo bora liko karibu kuja!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki