Kila Mtu Anaweza Kujifunza Kutokana na Video ya Noah—He Walked With God
Soma Mwanzo 6:1 hadi 9:19. Kisha itazame video ya Noah, na ufikirie jinsi unavyoweza kujibu maswali yafuatayo: (1) Ulimwengu ulikuwaje siku za Noa, na ulikujaje kuwa hivyo? (2) Ni nini kilichomfanya Noa awe mtu wa pekee sana, naye Mungu alimpa kazi gani, na kwa nini? (3) Huenda ikawa safina ilijengewa wapi, ujenzi ulichukua muda gani, na ilikuwa kubwa kadiri gani? (4) Mbali na kujenga safina, ni nini kingine ambacho Noa na familia yake walipaswa kufanya? (5) Unafikiri hali ilikuwaje ndani ya safina baada ya mlango kufungwa? (6) Ungehisije baada ya kuokoka Furiko? (7) Ni kikumbusho gani kuhusu Furiko ambacho twaona mara kwa mara, nacho chamaanisha nini? (8) Simulizi la Biblia kuhusu Noa lakufunza nini juu yako mwenyewe, familia yako, na kazi ambayo Mungu ametupa tufanye? (9) Ungependa kumwuliza Noa na familia yake maswali gani utakapokutana nao katika Paradiso? (10) Umepanga kutumiaje video ya Noah?