Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 2/03 uku. 7
  • Video Itakayokuelimisha na Kukutia Moyo!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Video Itakayokuelimisha na Kukutia Moyo!
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Shabaha ya Mashambulizi ya Sovieti
    Amkeni!—2001
  • Ukuzi Wenye Kutazamisha
    Amkeni!—1992
  • Jinsi Dini Ilivyoshambuliwa na Sovieti
    Amkeni!—2001
  • Twapelekwa Uhamishoni Siberia!
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2003
km 2/03 uku. 7

Video Itakayokuelimisha na Kukutia Moyo!

Mnamo Aprili 1951, Mashahidi wengi wa Yehova katika ule uliokuwa Muungano wa Sovieti walikusanywa wakiwa familia nzima-nzima, wakaingizwa kwenye mabehewa ya gari-moshi na kuhamishwa hadi Siberia. Kwa nini serikali yenye nguvu ya Sovieti iliazimia kuwamaliza? Ndugu zetu walivumiliaje na hata kuongezeka ijapokuwa waliteswa kikatili kwa miaka mingi? Utapata majibu kwenye video Faithful Under Trials—Jehovah’s Witnesses in the Soviet Union. Itazame, na acha ujumbe wake wenye kuelimisha ukutie moyo kudumisha uaminifu wako kwa Yehova, hata hali iweje!

Je, waweza kujibu maswali haya? (1) Mashahidi wa Yehova waliandikishwa kisheria lini kwa mara ya kwanza huko Urusi? (2) Familia za Mashahidi ziliongezekaje sana katika Muungano wa Sovieti, kabla na baada ya Vita ya Pili ya Ulimwengu? (3) Imani yao ilipinganaje na falsafa ya Lenin? (4) Mpango wa Operation North ulikuwa nini, na Stalin alikusudia kutimiza nini kupitia mpango huo? (5) Mashahidi waliohamishwa walipatwa na mambo gani, na waliambiwa wafanye nini ili wasihamishwe? (6) Ndugu na dada zetu walitianaje moyo na kuwashangaza maaskari kwenye safari yao ndefu hadi Siberia? (7) Mashahidi walivumilia magumu gani huko Siberia? (8) Watu wa Yehova walithamini sana maandalizi gani ya kiroho, na kwa nini? (9) Kwa nini ndugu zetu walikuwa tayari kuhatarisha maisha yao ili waweze kupokea vichapo, nao walifanikiwaje kushinda jitihada za wenye mamlaka za kuwazuia wasivipokee? (10) Khrushchev aliendelezaje mashambulizi juu ya watu wa Mungu? (11) Maofisa wa serikali walijaribuje kuvunja imani ya watoto wa Mashahidi? (12) Ndugu zetu walielewa nini waziwazi kuhusu sababu iliyofanya wateswe? (2002 Yearbook, ukurasa wa 203-204) (13) Mashambulizi makali ya watesaji yalisaidiaje tengenezo la Mungu badala ya kulimaliza? (2002 Yearbook, ukurasa wa 220-221) (14) Ni mambo gani yaliyotimizwa ambayo hapo awali yalikuwa ndoto tu kwa Mashahidi katika ule uliokuwa Muungano wa Sovieti? (15) Ni nini kilichowasaidia ndugu zetu kuvumilia majaribu, na sehemu ya mwisho ya video inaonyeshaje ukweli wa andiko la Yeremia 1:19? (16) Simulia jambo moja kati ya mambo yaliyoonwa kwenye video linaloonyesha uaminifu chini ya majaribu, ambalo hasa linakutia moyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki