Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 3/05 uku. 3
  • DVD Yenye Mafundisho Muhimu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • DVD Yenye Mafundisho Muhimu
  • Huduma ya Ufalme—2005
  • Habari Zinazolingana
  • “Unifundishe Kufanya Mapenzi Yako”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Yonathani—“Mwanamume Mmoja Katika Elfu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Sababu Yampasa Daudi Akimbie
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Kitabu Cha Biblia Namba 10—2 Samueli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Huduma ya Ufalme—2005
km 3/05 uku. 3

DVD Yenye Mafundisho Muhimu

DVD kumhusu Daudi (David—He Trusted in God) ina ujumbe gani? DVD hiyo inatufundisha kwamba ni lazima tumtegemee Yehova kama Daudi alivyofanya. (Zab. 91:2) Watoto na watu wazima wanaweza kujifunza kutokana na mfano wa Daudi kwa kutazama DVD hiyo inayohusu matukio muhimu ya maisha ya Daudi. (Zab. 31:14) Ili tufaidike zaidi, DVD hiyo ina sehemu ya maswali (“Video Quiz”) na ya misaada ya kujifunza (“Learning Activities”).

Tazama DVD hiyo, kisha ujiulize maswali yafuatayo: (1) Kwa nini Yehova alimchagua mfalme bora? (1 Sam. 15:10, 11; 16:1) (2) Kwa nini hakumchagua mmoja wa ndugu za Daudi? (1 Sam. 16:6, 7) (3) Kwa nini Sauli alitaka Daudi apige kinubi? (1 Sam. 16:14-23) (4) Goliathi alikuwa nani? (1 Sam. 17:4-10) (5) Kwa nini Daudi alitaka kupigana na Goliathi? (1 Sam. 17:23, 24, 36, 37) (6) Yonathani alikuwa nani? (1 Sam. 14:1) (7) Ni jambo gani lililomfanya Sauli awe adui mkubwa zaidi wa Daudi? (1 Sam. 18:25-29) (8) Kwa nini Daudi hakumwua Sauli? (1 Sam. 26:7-11) (9) Sauli alikufa kwa njia gani? (1 Sam. 31:1-6) (10) Daudi alifanya nini Yonathani alipokufa? (2 Sam. 1:11, 12) (11) Yehova alimwahidi Daudi nini? (2 Sam. 7:12, 13, 16) (12) Daudi alifanya kosa gani zito? (2 Sam. 11:1-5, 14-17) (13) Daudi alionyeshaje kwamba alisikitika sana kwa sababu ya kosa alilofanya? (Zab. 51) (14) Daudi alimfundisha kijana Sulemani nini? (1 Fal. 2:1-4; 1 Nya. 22:6-13; 28:9, 10) (15) Utawala wa Yesu utawanufaishaje Daudi na Yonathani, nao utakunufaishaje?—Isa. 11:6-9; Yoh. 11:25, 26.

Hebu fikiria: Unaweza kumtegemea Mungu kama Daudi kwa njia gani?

Enyi wazazi, wafundisheni watoto wenu umuhimu wa kumtegemea Mungu, kama Daudi alivyofanya.—Zab. 56:11.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki