Mfano Mzuri kwa Vijana na Wazee
Alikuwa na uhusiano wa karibu pamoja na Mungu. Alitumia maisha yake kufanya mapenzi ya Yehova. “Alitembea pamoja na Mungu wa kweli” na akabarikiwa kwa kufanya hivyo. Mtu huyo aliitwa Noa, naye ni mfano unaofaa kuigwa na vijana na vilevile wazee. (Mwa. 6:9) Video Noah—He Walked With God itakusaidia kuwazia jinsi maisha ya Noa yalivyokuwa, sababu iliyofanya astahili baraka za Yehova, na jinsi unavyoweza kuiga sifa zake nzuri. Mahali ambapo hakuna video, kuchunguza Mwanzo sura ya 6 hadi 9 kutatutia moyo kuiga mfano mzuri ambao Noa aliwawekea Wakristo wa kweli katika siku hizi za mwisho.
DVD ya Noah ina maswali yafuatayo. Tazama video hiyo, au ikiwa haipatikani katika eneo lenu, soma maandiko yaliyotajwa hapa kuanzia Mwanzo sura ya 6 hadi 9 kisha ujiulize: (1) Malaika fulani walifanya kosa gani, nao Wanefili walikuwa nani? (Mwa. 6:1, 2, 4) (2) Kwa nini watu walikuwa wabaya sana, naye Mungu alihisije kuhusu hilo? (Mwa. 6:4-6) (3) Noa alitofautianaje nao? (Mwa. 6:22) (4) Waovu waliangamizwaje? (Mwa. 6:17) (5) Safina ilikuwa kubwa kadiri gani? (Mwa. 6:15) (6) Noa alifanya nini kingine, nao watu walitendaje? (Mt. 24:38, 39; 2 Pet. 2:5) (7) Ni wanyama wangapi wa kila aina walioingia ndani ya safina? (Mwa. 7:2, 3, 8, 9) (8) Kulinyesha kwa siku ngapi, nayo dunia ilifunikwa na maji kwa muda gani? (Mwa. 7:11, 12; 8:3, 4) (9) Kwa nini Noa na familia yake waliokoka? (Mwa. 6:18, 22; 7:5) (10) Safina ilitua wapi? (Mwa. 8:4) (11) Noa alijuaje kwamba ilikuwa salama kutoka kwenye safina? (Mwa. 8:6-12) (12) Noa alifanya nini alipotoka kwenye safina? (Mwa. 8:20-22) (13) Upinde wa mvua unawakilisha nini? (Mwa. 9:8-16) (14) Inamaanisha nini ‘kutembea pamoja na Mungu’? (Mwa. 6:9, 22; 7:5) (15) Tunapaswa kufanya nini ili tumwone Noa katika Paradiso? (Mt. 28:19, 20; 1 Pet. 2:21)
Simulizi la Biblia kuhusu Noa ambaye alikuwa mwaminifu na mtiifu, limekufundisha nini kuhusu jinsi ambavyo wewe pia unaweza ‘kutembea pamoja na Mungu’ na kuwa na uhakika katika nguvu za Yehova za kuwaokoa watu wake wa siku hizi?—Mwa. 7:1; Met. 10:16; Ebr. 11:7; 2 Pet. 2:9.