Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/10 uku. 3
  • Unapohitaji Vitabu vya Lugha ya Kigeni kwa Uharaka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unapohitaji Vitabu vya Lugha ya Kigeni kwa Uharaka
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoa Vichapo Katika Eneo Lenye Lugha Mbalimbali
    Huduma Yetu ya Ufalme—2003
  • Tovuti Yetu Rasmi—Itumie Kumhubiria Mtu Anayezungumza Lugha Tofauti
    Huduma Yetu ya Ufalme—2012
  • Habari Inayowasaidia Watu
    Huduma Yetu ya Ufalme—2004
  • Tovuti Yetu Rasmi—Itumie Katika Huduma Yako
    Huduma Yetu ya Ufalme—2012
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2010
km 10/10 uku. 3

Unapohitaji Vitabu vya Lugha ya Kigeni kwa Uharaka

Wakati mwingine tunakutana na watu ambao wanapenda kusoma vitabu vyetu katika lugha ya kigeni ambayo haipatikani kutanikoni. Je, unajua kwamba ukiwa mahali ambapo kuna Intaneti na printa, unaweza kuchapa habari zilizo katika vitabu vyetu katika lugha 400 hivi? Unaweza kufanya hivyo kwa kufuata maagizo yafuatayo:

• Tembelea www.watchtower.org, kituo chetu rasmi cha Intaneti.

• Kwenye upande wa kulia wa ukurasa kaya kuna orodha fupi ya lugha mbalimbali. Bofya picha ya tufe la dunia ili upate orodha nzima ya lugha zote zinazopatikana.

• Bofya lugha unayotaka. Ukurasa utatokea unaoonyesha habari unazoweza kuchapa, kama vile trakti, broshua, na makala mbalimbali. Kwa kuwa ukurasa huo umeandikwa katika lugha ambayo umechagua, usiwe na wasiwasi usipoelewa vichwa vilivyomo.

• Bofya kipengee chochote cha habari unazotaka. Habari zitatokea kwenye skrini na zinaweza kuchapwa moja kwa moja kutoka kwa kompyuta.

Kituo chetu cha Intaneti kina habari chache tu; vitabu zaidi vinapatikana kupitia kutaniko. Mtu aliyehubiriwa anapoonyesha kupendezwa zaidi, ni bora kuagiza vitabu kupitia kutaniko.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki