Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb18 Agosti uku. 3
  • Mkumbuke Mke wa Loti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mkumbuke Mke wa Loti
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Mkumbuke Mke wa Loti
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Mke wa Lutu Alitazama Nyuma
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Tayarisha kwa Ajili ya Kukombolewa Kuingia Ndani ya Ulimwengu Mpya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Nilikuwa Maskini​—Sasa Ni Tajiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
mwb18 Agosti uku. 3
Mke wa Loti akitazama nyuma kuelekea Sodoma na kugeuka nguzo ya chumvi

MAISHA YA MKRISTO

Mkumbuke Mke wa Loti

Kwa nini mke wa Loti alitazama nyuma alipokuwa akikimbia kutoka Sodoma? Biblia haisemi. (Mwa 19:17, 26) Muktadha wa onyo la Yesu unaonyesha kwamba huenda alitamani vitu alivyoacha nyuma. (Lu 17:31, 32) Tunaweza kufanya nini ili tusipoteze kibali cha Mungu kama mke wa Loti alivyofanya? Hatupaswi kuruhusu jitihada za kutafuta mali ziwe jambo kuu maishani. (Mt 6:33) Yesu alifundisha kwamba hatuwezi “kutumikia Mungu na Utajiri.” (Mt 6:24) Lakini vipi tukitambua kwamba vitu vya kimwili vimeanza kutukengeusha tuache kutanguliza mambo ya kiroho? Tunaweza kumwomba Yehova ufahamu utakaotuwezesha kuona mabadiliko tunayohitaji kufanya na pia tumwombe ujasiri na nguvu za kufanya mabadiliko hayo.

KUMBUKENI VIDEO YENYE SEHEMU TATU YENYE KICHWA MKUMBUKE MKE WA LOTI, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Anna akiwa kazini; Gloria akiwa na mjomba wake; Brian na Gloria wakisali pamoja

    Ninaweza kuonyeshaje kupitia matendo yangu kwamba ‘ninamkumbuka mke wa Loti’?

    Shinikizo la kutafuta pesa nyingi zaidi liliathirije mawazo, maneno, na matendo ya Gloria?

  • Mke wa Loti ni kielelezo cha kuonya kwetu leo katika njia zipi?

  • Joe na familia yake walifaidikaje kwa kutumia kanuni za Biblia?

  • Watu ambao Anna alishirikiana nao kazini waliathirije hali yake ya kiroho?

  • Kwa nini tunahitaji kuwa na ujasiri tunaposhinikizwa kutanguliza pesa?

  • Brian na Gloria walifanya nini ili kutanguliza tena mambo ya kiroho maishani mwao?

  • Uliona kanuni gani za Biblia zikitumiwa katika video hiyo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki