Mabinti wa Selofehadi wakiomba urithi wa baba yao
HAZINA ZA NENO LA MUNGU
Mwige Yehova kwa Kutokuwa na Ubaguzi
Mabinti watano wa Selofehadi waliomba waruhusiwe kuhifadhi urithi wa baba yao (Hes 27:1-4; w13 6/15 10 ¶14; ona picha kwenye jalada)
Yehova alifanya uamuzi usio na ubaguzi (Hes 27:5-7; w13 6/15 11 ¶15)
Sisi pia tunapaswa kutenda bila ubaguzi (Hes 27:8-11; w13 6/15 11 ¶16)
Tunaiga sifa ya Yehova ya kutokuwa na ubaguzi kwa kuwatendea waamini wenzetu kwa heshima na upendo mshikamanifu na kwa kuwahubiria watu wa malezi yote.