Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb22 Mei uku. 7
  • Je, Uko Tayari Kukabiliana na Misukosuko ya Kijamii?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Uko Tayari Kukabiliana na Misukosuko ya Kijamii?
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Umejitayarisha?
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
  • Endelea Kuwa Tayari Katika Sehemu ya Mwisho ya “Siku za Mwisho”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2021
  • “Je, Umejitayarisha Kukabiliana na Kuporomoka kwa Uchumi?”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma​—Kuwafundisha Wanafunzi Wetu Kujitayarisha
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
mwb22 Mei uku. 7
Familia ikitazama habari kuhusu msukosuko wa kijamii kwenye TV. Mikoba yao ya dharura iko karibu.

MAISHA YA MKRISTO

Je, Uko Tayari Kukabiliana na Misukosuko ya Kijamii?

Kadiri mwisho wa mfumo huu unavyokaribia, tunatarajia kwamba misukosuko ya kijamii, ugaidi, na vita vitaongezeka. (Ufu 6:4) Tunaweza kujitayarishaje kwa ajili ya hali ngumu za wakati ujao?

  • Jitayarishe kiroho: Tafuta kanuni na masimulizi ya Biblia ambayo yataimarisha tumaini lako katika Yehova na tengenezo lake na ambayo yatakusaidia kudumisha msimamo wa kutounga mkono upande wowote. (Met 12:5; jr 125-126 ¶23-24) Sasa ndio wakati wa kuimarisha urafiki pamoja na wengine ndani ya kutaniko.​—1Pe 4:7, 8

  • Jitayarishe kimwili: Pangeni jinsi ya kuhakikisha mko salama ikiwa hamwezi kutoka nyumbani na mhifadhi mahitaji muhimu. Pia, pangeni mambo mtakayofanya ikiwa mtalazimika kuondoka nyumbani. Kagueni vitu vilivyo ndani ya mkoba wa dharura, na mtie ndani pesa na vitu vya kujikinga kama vile glavu na barakoa. Fahamu jinsi ya kuwasiliana na wazee, na uwe na uhakika wao wanafahamu jinsi ya kuwasiliana nawe.​—Isa 32:2; g17.5 3-7

Wakati wa msukosuko, dumisha ratiba yako ya kiroho. (Flp 1:10) Epuka kuhamahama isipokuwa iwe lazima. (Mt 10:16) Shiriki na wengine chakula na mahitaji mengine.​—Ro 12:13.

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA JE, UMEJITAYARISHA KUKABILIANA NA MAJANGA? KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Yehova anaweza kutusaidiaje wakati wa majanga?

  • Tunaweza kuchukua hatua zipi zinazofaa ili kujitayarisha?

  • Tunaweza kuwasaidiaje wengine ambao wameathiriwa na majanga?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki