Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb22 Mei uku. 11
  • Dhibiti Tamaa Zako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Dhibiti Tamaa Zako
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Habari Zinazolingana
  • Unaweza Kuyavunja Mazoea ya Tumbako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Kuvuta Sigara na Kutumia Sigara za Kielektroni?
    Vijana Huuliza
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Kuvuta Sigara?
    Amkeni!—2011
  • Mungu ana maoni gani kuhusu Kuhusu Kuvuta Sigara?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
mwb22 Mei uku. 11

MAISHA YA MKRISTO

Dhibiti Tamaa Zako

Tukiwa wanadamu wasio wakamilifu, lazima tupambane kila wakati ili kudhibiti tamaa zetu. Tukiziruhusu zitutawale, tunaweza kupoteza kibali cha Yehova. Kwa mfano, watu fulani huruhusu tamaa ya chakula, mavazi, na makao izidi upendo wao kwa Yehova. Wengine hutosheleza tamaa yao ya ngono bila kuzingatia viwango vya Mungu. (Ro 1:26, 27) Wengine hukubali kushinikizwa na marafiki kwa sababu wanatamani kupendwa au kukubaliwa na wengine.​—Kut 23:2.

Tunawezaje kudhibiti tamaa zetu? Tunapaswa kufanya yote tuwezayo ili kukazia fikira mambo ya kiroho. (Mt 4:4) Pia, tunapaswa kumsihi Yehova atusaidie kudhibiti tamaa zetu. Kwa nini? Kwa sababu anajua kinachotufaa na anajua jinsi ya kutosheleza tamaa zetu zinazofaa.​—Zb 145:16.

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA USIRUHUSU MAISHA YAKO YAATHIRIWE NA SIGARA, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Picha kutoka kwenye video “Usiruhusu Maisha Yako Yaathiriwe na Sigara.” Kiwanda kikitokeza midoli inayovuta sigara.

    Kwa nini watu huvuta sigara?

  • Picha kutoka kwenye video “Usiruhusu Maisha Yako Yaathiriwe na Sigara.” Mapafu ya mvuta-sigara yakikohoa kwa nguvu.

    Kuvuta sigara kunaweza kuwa na madhara gani kwako?

  • Picha kutoka kwenye video “Usiruhusu Maisha Yako Yaathiriwe na Sigara.” Mfanyabiashara mkubwa sana akining’iniza sigara ya kielektroni kama chambo kwenye ndoano mbele ya msichana.

    Kwa nini ni vibaya kuvuta sigara, kutia ndani zile za kielektroni?​—2Ko 7:1

  • Picha kutoka kwenye video “Usiruhusu Maisha Yako Yaathiriwe na Sigara.” Msichana akiwa juu ya paa la jengo akitazama anga jangavu lenye jua.

    Unaweza kushinda tamaa ya kuvuta sigara!

    Unaweza kufanya nini ili kukataa kuvuta sigara au kuacha zoea hilo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki