Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w22 Machi uku. 13
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Habari Zinazolingana
  • Mefiboshethi Mwanamume Mwenye Kuthamini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Je, Umewahi Kuhisi Kama Umetengwa na Wengine?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Yonathani Alikuwa jasiri na Mshikamanifu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • “Wakashikamana na Kuwa Marafiki wa Karibu Sana”
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
w22 Machi uku. 13

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Kwa nini andiko la 2 Samweli 21:7-9 linasema kwamba Daudi ‘alimhurumia Mefiboshethi’ na kisha akaruhusu Mefiboshethi auawe?

Baadhi ya watu wanaosoma simulizi hilo haraka-haraka wamejiuliza swali hilo. Lakini mistari hiyo inazungumzia wanaume wawili walioitwa Mefiboshethi, na tunaweza kujifunza jambo fulani kuhusu kilichotokea.

Mfalme Sauli wa Israeli alikuwa na wana saba na binti wawili. Mwana wa kwanza wa Sauli alikuwa Yonathani. Baadaye, mfalme alipata mwana aliyeitwa Mefiboshethi, aliyemzaa na suria aliyeitwa Rispa. Inashangaza kwamba Yonathani pia alikuwa na mwana aliyeitwa Mefiboshethi. Hivyo, Mfalme Sauli alikuwa na mwana aliyeitwa Mefiboshethi, na mjukuu aliyeitwa jina hilo pia.

Pindi fulani, Mfalme Sauli alianza kuwashambulia Wagibeoni walioishi miongoni mwa Waisraeli na alitaka kuwaangamiza. Inaonekana baadhi yao waliuawa. Ni wazi kwamba hilo lilikuwa kosa. Kwa nini? Kwa sababu katika siku za Yoshua, wakuu wa Israeli walikuwa wamefanya agano la amani pamoja na Wagibeoni.​—Yos. 9:3-27.

Bado agano hilo lilikuwa linaendelea katika siku za Mfalme Sauli. Mfalme alitenda kinyume na agano hilo kwa kujaribu kuwaangamiza Wagibeoni. Shambulizi hilo lilitokeza ‘hatia ya damu juu ya Sauli na nyumba yake.’ (2 Sam. 21:1) Hatimaye, Daudi akawa mfalme. Wagibeoni waliookoka walimwambia kuhusu kosa hilo baya. Daudi aliwauliza jinsi ambavyo kosa hilo zito la Sauli lingeweza kufunikwa na hivyo kufungua njia ili Yehova abariki nchi yao. Badala ya kuomba pesa, Wagibeoni waliomba wana saba wa mwanamume ambaye “alipanga njama ya kuwaangamiza” wauawe. (Hes. 35:30, 31) Daudi alikubali ombi lao.​—2 Sam. 21:2-6.

Wakati huo, Sauli na Yonathani walikuwa wamekufa vitani, lakini Mefiboshethi, mwana wa Yonathani alikuwa hai. Alipata ulemavu utotoni kutokana na tukio ambalo halikuhusiana na shambulizi la babu yake dhidi ya Wagibeoni. Daudi alikuwa amefanya agano la urafiki pamoja na Yonathani, ambalo lingewanufaisha wazao wao, kutia ndani Mefiboshethi, mwana wa Yonathani. (1 Sam. 18:1; 20:42) Simulizi hilo linasema: “Mfalme [Daudi] akamhurumia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa sababu ya kiapo ambacho Daudi na Yonathani mwana wa Sauli walikuwa wameapiana mbele za Yehova.”​—2 Sam. 21:7.

Hata hivyo, Daudi alikubali kutimiza ombi la Wagibeoni. Akawapa Wagibeoni wana wawili wa Sauli, ambao mmoja wao aliitwa Mefiboshethi, na wajukuu watano wa Sauli. (2 Sam. 21:8, 9) Hatua hiyo ambayo Daudi alichukua iliondoa hatia ya damu katika nchi.

Tunaweza kujifunza mengi kutokana na simulizi hilo. Sheria ya Mungu iko wazi. Ilisema hivi: “Wana hawapaswi kuuawa kwa sababu ya dhambi za baba zao.” (Kum. 24:16) Yehova hangeruhusu jambo lililowapata wana wawili na wajukuu watano wa Sauli litokee ikiwa hawangekuwa na hatia. Sheria hiyo iliongeza hivi: “Mtu anapaswa kuuawa kwa sababu ya dhambi yake mwenyewe.” Inaonekana kwamba wazao saba wa Sauli waliokufa, walikuwa wameshiriki kwa njia fulani katika jaribio la Sauli la kuwaangamiza Wagibeoni. Matokeo ni kwamba wote saba walikufa kwa sababu ya makosa yao.

Simulizi hili linaonyesha kwamba mtu hawezi kujitetea anapofanya kosa kwa kufikiri au kusema kwamba alikuwa anafuata maagizo. Methali moja yenye hekima inasema hivi: “Lainisha mapito ya miguu yako, na njia zako zote zitakuwa thabiti.”​—Met. 4:24-27; Efe. 5:15.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki