Madhara ya Vita
Vita na ukatili ni moja kati ya mambo yanayosababisha maumivu makali sana kwa watu. Wanajeshi na raia wengi walioathiriwa na vita wanajua madhara yanayosababishwa na vita.
WANAJESHI
“Mara nyingi, unaona watu waliokuzunguka wakiuawa au kujeruhiwa vibaya. Kila mara unahofia usalama wako.”—Gary, Uingereza.
“Nilipigwa risasi mgongoni na usoni, na niliona watu wengi wakiuawa, kutia ndani watoto na wazee. Vita inafanya moyo wako kuwa mgumu.”—Wilmar, Kolombia.
“Mtu anapopigwa risasi mbele yako, ni vigumu sana kusahau jambo hilo. Akilini mwako unaendelea kusikia kelele za mtu huyo akipigania uhai wake. Huwezi kamwe kumsahau mtu huyo.”—Zafirah, Marekani.
RAIA
“Nilihisi kwamba nisingeweza kuwa na furaha tena. Unahofia uhai wako, lakini unahofia hata zaidi uhai wa familia yako na marafiki.”—Oleksandra, Ukrainia.
“Inaogopesha sana kusimama kwenye foleni kwa ajili ya chakula kuanzia saa 8:00 usiku hadi saa 5:00 usiku, ukihofia kwamba utapigwa risasi.”—Daler, Tajikistan.
“Vita vilisababisha wazazi wangu wauawe. Nilibaki nikiwa yatima bila mtu wa kunifariji au wa kunitunza.”—Marie, Rwanda.
Licha ya matokeo mabaya ya vita, watu wanaotajwa hapo juu wamepata amani. Zaidi ya hilo, wana uhakika kwamba vita na ukatili vitakwisha hivi karibuni. Toleo hili la Mnara wa Mlinzi litatumia Biblia kueleza jinsi jambo hilo litakavyotukia.