Utendaji Wa Mashahidi Wa Yehova Katika Nyakati Za Kisasa
Moldova
Kwa zaidi ya miaka 60, Mashahidi wa Yehova nchini Moldova waliteseka chini ya utawala wa wafalme Warumania, utawala wa Ufashisti, na Ukomunisti. Walipingwa pia na Kanisa Othodoksi wakati wa utawala wa wafalme Warumania na utawala wa Ufashisti. Licha ya hayo yote, idadi ya watu ambao kila Shahidi anapaswa kuhubiria nchini Moldova ni ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine. Soma jinsi ambavyo Yehova huwaimarisha wote wanaomwogopa, na kuwapa ushindi wote ambao husimama imara bila kuwaogopa wanadamu.
Nchi Mbili za Kongo
Wewe hufikiria nini jina “Kongo” linapotajwa? Wengi hufikiria msitu mkubwa sana wenye joto kali ambao haupenywi na mwangaza wa jua. Unasikia sauti za tumbili na ndege mbalimbali na milio ya ngoma yenye ujumbe kutoka vijiji vya mbali. Huenda ukawazia mto mkubwa sana wenye matope, unaojipinda-pinda polepole kama nyoka mkubwa katikati ya Afrika. Lakini si hayo tu, kuna mambo mengi zaidi katika nchi za Kongo. Nchi hizo mbili huitwa kwa jina la mto unaozitenganisha. Imani yako itaimarika unaposoma jinsi wanaume na wanawake jasiri walivyoeneza kweli za Biblia katika eneo hilo lenye kuvutia.