Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb15 uku. 28-uku. 29 fu. 1
  • Kuweka Wakfu Ofisi ya Tawi ya Sri Lanka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuweka Wakfu Ofisi ya Tawi ya Sri Lanka
  • 2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Habari Zinazolingana
  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kuishinda Miito Migumu ya Maisha Katika Asia ya Kusini
    Amkeni!—1994
  • Elimu Ambayo Imeendelea Katika Maisha Yangu Yote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Kuwekwa Wakfu kwa Ofisi za Tawi
    2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb15 uku. 28-uku. 29 fu. 1
Picha katika ukurasa wa 28

MATUKIO MUHIMU YA MWAKA ULIOPITA

Kuweka Wakfu Ofisi ya Tawi ya Sri Lanka

Ramani katika ukurasa wa 29

NDUGU na dada wa Sri Lanka waliovalia mavazi ya kitamaduni waliwakaribisha kwa uchangamfu wajumbe 130 kutoka nchi 19, waliohudhuria kuwekwa wakfu kwa ofisi ya tawi katika kisiwa maridadi cha Sri Lanka. Kikundi cha watoto kiliimba nyimbo za Ufalme, na kila mtu alifurahia vitu mbalimbali vya kitamaduni vyenye kuvutia, vyakula vitamu vya kienyeji, muziki wenye kuchangamsha, pamoja na ushirika mchangamfu wa Kikristo.

Majengo mapya na yale yaliyokarabatiwa katika ofisi hiyo ya tawi yaliwekwa wakfu kwa Yehova Jumamosi, Januari 11, 2014. Watu 893 walisikiliza kwa makini programu katika lugha tatu. Watu walishangilia kwa kupiga makofi kwa muda mrefu ndugu Mark Sanderson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza alipouliza hivi: “Je, mngependa kuyaweka wakfu kwa Yehova Mungu majengo haya mapya?”

Siku iliyofuata, watu wengine 7,701 walikusanyika ili kusikiliza rekodi ya programu hiyo pamoja na hotuba yenye kutia moyo iliyotolewa na Ndugu Sanderson. Maeneo matano ya nchi hiyo yaliunganishwa kupitia Intaneti ili kusikiliza programu hiyo. Kwa mara ya kwanza, video ya Intaneti iliwawezesha ndugu na dada katika maeneo yote ya kisiwa hicho kuwaona na kuwasikia wenzao wakiimba nyimbo za Ufalme. Tukio hilo la kihistoria kwa kweli liliwaletea “shangwe kubwa.”—Neh. 12:43.

Picha katika ukurasa wa 29
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki