12 Kwa hiyo wanaume waliokuwa kwenye kituo hicho cha ulinzi wakamwambia Yonathani na mtumishi wake aliyembebea silaha: “Njooni hapa juu tulipo, nasi tutawafunza somo!”+ Mara moja Yonathani akamwambia hivi mtumishi aliyembebea silaha: “Nifuate, kwa kuwa Yehova atawatia mikononi mwa Waisraeli.”+