22 Kisha wakaaji wa Yerusalemu wakamweka Ahazia mwanawe wa mwisho kuwa mfalme baada yake, kwa maana kundi la wavamizi lililokuja kambini pamoja na Waarabu lilikuwa limewaua wana wote wakubwa wa Yehoramu.+ Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu akaanza kutawala akiwa mfalme wa Yuda.+