6 Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa,+ na kwa hiyo mfalme akaingia ndani kumwona. Ndipo Amnoni akamwambia mfalme: “Tafadhali, acha Tamari dada yangu aingie ndani, aniokee keki mbili zenye umbo la moyo chini ya macho yangu, ili nile mkate kama mgonjwa kutoka mkononi mwake.”