WIMBO NA. 11
Uumbaji Unamsifu Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Ee Yehova, wastahili sifa.
Mbingu zako zinakutukuza.
Uumbaji unakutangaza;
Wasikiwa duniani kote.
Uumbaji unakutangaza;
Wasikiwa duniani kote.
2. Ili tuwe na hekima kweli,
Ni lazima tukuhofu wewe.
Amri zako zatuelimisha,
Na ni bora kuliko dhahabu.
Amri zako zatuelimisha,
Na ni bora kuliko dhahabu.
3. Kukujua, hutupa kusudi.
Neno lako, hutupa uhai.
Walitakasao jina lako,
Wana pendeleo kubwa sana.
Walitakasao jina lako,
Wana pendeleo kubwa sana.
(Ona pia Zab. 12:6; 89:7; 144:3; Rom. 1:20.)