WIMBO NA. 6
Mbingu Zatangaza Utukufu wa Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Mbingu, nyota, zamtukuza Mungu.
Uumbaji wake,
angani twaona.
Kila siku, wamsifu Mungu.
Fahari na nguvu zake,
mwezi watangaza.
2. Sheria ya Yehova ni kamili.
Vikumbusho vyake,
huongoza wote.
Maamuzi yake yanafaa.
Neno lake ni hakika,
sheria ni safi.
3. Kumwogopa Yehova kwastahili.
Nazo amri zake,
zapita dhahabu.
Maagizo yake hutulinda.
Jina lake takatifu
tunalitukuza.
(Ona pia Zab. 111:9; 145:5; Ufu. 4:11.)