Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unaweza Kumpata Ndugu Yako
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Oktoba 15
    • Lakini, muktadha wadokeza kwamba ni lazima Yesu alimaanisha dhambi nzito. Ilikuwa nzito kiasi cha kwamba ingeweza kufanya mkosaji aonwe “kama vile mtu wa mataifa na kama mkusanya-kodi.” Maneno hayo yadokeza nini?

      6 Wanafunzi wa Yesu waliosikia maneno hayo walijua kwamba Wayahudi wenzao hawakuwa na shughuli na watu wasio Wayahudi. (Yohana 4:9; 18:28; Matendo 10:28) Nao bila shaka waliwaepuka wakusanya-kodi, wanaume Wayahudi ambao waligeuka wakawa wanawadhulumu watu. Basi andiko la Mathayo 18:15-17 lilikuwa likirejezea hasa dhambi nzito, si kuumizwa au makosa madogo-madogo ya kibinafsi ambayo unaweza kusamehe tu na kusahau.—Mathayo 18:21, 22.a

  • Unaweza Kumpata Ndugu Yako
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Oktoba 15
    • a Kitabu Cyclopedia cha McClintock na Strong chasema: “Wakusanya-kodi wa Agano Jipya walionwa kuwa wahaini na waasi-imani, waliochafuliwa kwa kuchangamana sana na wapagani, na walio tayari kutumiwa na waonezi. Wao walionwa kuwa sehemu ya watenda-dhambi . . . Wakiwa wametengwa, watu wenye heshima waliwaepuka, na rafiki zao au waandamani wao wa pekee walikuwa watu ambao pia walikuwa wametengwa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki