Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • Tukifundisha vibaya, huenda matokeo yakawa yenye kusikitisha. Paulo alionya: “Kazi ya yeyote ambayo ameijenga juu ya huo ikibaki, atapokea thawabu; kazi ya yeyote ikichomwa kabisa, atapata hasara, lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini, ikiwa ndivyo, itakuwa ni kama kupitia moto.”c—1 Wakorintho 3:14, 15.

      14. (a) Huenda wafanya-wanafunzi Wakristo ‘wakapataje hasara,’ hata hivyo huenda wao wakafikiaje wokovu kama kupitia moto? (b) Tunaweza kupunguzaje hatari ya kupata hasara?

      14 Ni maneno yenye kuamsha fikira kama nini! Inaweza kuumiza sana kujitahidi kusaidia mtu awe mwanafunzi, kisha kumwona huyo mtu akishindwa na jaribu au mnyanyaso na hatimaye kuacha ile kweli. Paulo anakubaliana na jambo hilo anaposema kwamba sisi hupata hasara katika visa kama hivyo. Jambo hilo linaweza kuwa lenye kuumiza sana hivi kwamba wokovu wetu unafafanuliwa kuwa ‘kama unapitia moto’—kama mtu aliyepoteza kila kitu motoni, naye mwenyewe akaponea chupuchupu. Tunaweza kupunguzaje hatari ya kupata hasara upande wetu? Jenga kwa vifaa vidumuvyo! Tukiwafundisha wanafunzi wetu ili kuwafikia mioyo, tukiwachochea wathamini sifa za Kikristo kama vile hekima, ufahamu, kumhofu Yehova, na imani ya kweli, basi tunajenga kwa vifaa vyenye kudumu, visivyoweza kushika moto. (Zaburi 19:9, 10; Mithali 3:13-15; 1 Petro 1:6, 7) Wanaojipatia sifa hizo wataendelea kufanya mapenzi ya Mungu; nao wana tumaini hakika la kuendelea kuwa hai milele. (1 Yohana 2:17)

  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • c Paulo alishuku kuokoka kwa “kazi” ya mjenzi wala si mjenzi mwenyewe. Tafsiri ya The New English Bible yatafsiri mstari huo hivi: “Jengo la mtu likistahimili, atapokea thawabu; likichomeka, atapata hasara; na bado ataponyoka na uhai wake, kama vile mtu aponyokavyo kutoka motoni.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki