-
Ule Uasi-imani Mkubwa WasitawiMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Miongoni mwa mikengeuko ya mapema kabisa kulikuwa na kutenganishwa kwa maneno “mwangalizi” (Kigiriki, e·piʹsko·pos) na “mwanamume mzee,” au “mzee” (Kigiriki, pre·sbyʹte·ros), hivi kwamba maneno hayo hayakutumiwa tena kurejezea cheo kilekile kimoja cha daraka. Mwongo mmoja hivi baada ya kifo cha mtume Yohana, Ignatius, “askofu” wa Antiokia, katika barua yake kwa Wasmirna, aliandika hivi: “Hakikisheni kwamba mwamfuata askofu [mwangalizi], kama Yesu Kristo amfuatavyo Baba, na presbiteri [baraza la wanaume wazee] kama kwamba mnafuata wale Mitume.” Hivyo Ignatius alitetea maoni ya kwamba kila kutaniko lapasa kusimamiwa na askofu mmoja,c au mwangalizi, ambaye alipaswa kutambuliwa kuwa tofauti, na mwenye mamlaka kubwa kuliko, wapresbiteri, au wanaume wazee.
Ingawa hivyo, kutenganishwa huko kulitokeaje? Augustus Neander katika kitabu chake, The History of the Christian Religion and Church, During the Three First Centuries, aeleza wazi lililotukia: “Katika karne ya pili . . . , ni lazima iwe ndipo cheo cha sasa cha msimamizi mkuu wa kuchaguliwa wa wapresbiteri kilipofanyizwa, ambaye, kwa sababu ndiye hasa aliyekuwa na uangalizi wa kila kitu, alipewa lile jina la [e·piʹsko·pos], na hapo akatofautishwa na wale wapresbiteri wengine wote.”
Hivyo msingi uliwekwa ili jamii ya makasisi iibuke hatua kwa hatua. Karibu karne moja baadaye, Cyprian, “askofu” wa Carthage, Afrika Kaskazini, alikuwa mtetezi imara wa mamlaka ya maaskofu—kuwa kikundi tofauti na wapresbiteri (ambao baadaye walijulikana kuwa makuhani au mapadrid), na mashemasi, na watu wa kawaida. Lakini yeye hakupendelea umashuhuri wa askofu mmoja juu ya wengine.e
-
-
Ule Uasi-imani Mkubwa WasitawiMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
c Neno la Kiingereza “bishop” (askofu) hutokana na neno la Kigiriki e·piʹsko·pos (“mwangalizi”) kama ifuatavyo: kutokana na neno bisshop la Kiingereza cha Enzi ya Katikati, lililotokana na neno bisceop la Kiingereza cha Zamani, lililotokana na neno biscopus, la Kilatini cha watu wa kawaida, ambalo ni namna tofauti ya neno episcopus la Kilatini cha Baadaye, lililotokana na neno la Kigiriki e·piʹsko·pos.
-
-
Ule Uasi-imani Mkubwa WasitawiMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
d Neno la Kiingereza “priest” (kuhani au padri) latokana na pre·sbyʹte·ros (“mwanamume mzee,” au “mzee”) kama ifuatavyo: kutokana na neno pre(e)st la Kiingereza cha Enzi ya Katikati, lililotokana na neno prēost la Kiingereza cha Zamani, lililotokana na neno prester la Kilatini cha watu wa kawaida, lililofupishwa kutokana na neno presbyter la Kilatini cha Baadaye, lililotokana na pre·sbyʹte·ros la Kigiriki.
-