-
Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
-
-
kazi ya kila mmoja itakuwa dhahiri, kwa maana ile siku itaifichua, kwa sababu itafunuliwa kwa njia ya moto; na moto wenyewe utathibitisha ni ya namna gani kazi ya kila mmoja.” (1 Wakorintho 3:12, 13)
-
-
Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
-
-
11 Ni nini ambacho kingeyapata majengo hayo yakishika moto? Jibu lilikuwa wazi siku ya Paulo kama lilivyo siku yetu. Kwa kweli, huko nyuma mwaka wa 146 K.W.K., jiji la Korintho lilikuwa limeshindwa na kuwashwa moto na Jenerali Mummius wa Roma. Kwa kweli, majengo mengi ya mbao, nyasi kavu, au bua yaliharibiwa kabisa. Vipi majengo imara ya mawe yaliyokuwa yamepambwa kwa fedha na dhahabu? Hapana shaka haya yaliokoka. Huenda ikawa wanafunzi wa Paulo huko Korintho walipitia karibu na majengo hayo kila siku—majengo ya mawe yenye fahari yaliyookoka misiba ambayo zamani ilikuwa imeharibu majengo ya muda yaliyokuwa karibu. Paulo alidhihirisha hoja yake kwa mkazo ulioje! Tunapofundisha twahitaji kujiona kuwa wajenzi. Twataka kutumia vifaa bora zaidi na vyenye kudumu zaidi iwezekanavyo. Kwa njia hiyo, yaelekea zaidi kwamba kazi yetu itadumu. Vifaa hivyo vyenye kudumu ni vipi, na kwa nini ni muhimu kuvitumia?
-
-
Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
-
-
Haingeokoka “moto.” Paulo alikuwa akizungumzia moto upi?
13. Moto katika kielezi cha Paulo wawakilisha nini, na yawapasa Wakristo wote wajue nini?
13 Kuna moto ambao sisi sote hukabili maishani—majaribu ya imani yetu. (Yohana 15:20; Yakobo 1:2, 3) Kama vile tunavyohitaji kujua leo, Wakristo katika Korintho walihitaji kujua kwamba kila mtu tunayefundisha kweli atajaribiwa. Tukifundisha vibaya, huenda matokeo yakawa yenye kusikitisha. Paulo alionya: “Kazi ya yeyote ambayo ameijenga juu ya huo ikibaki, atapokea thawabu; kazi ya yeyote ikichomwa kabisa, atapata hasara, lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini, ikiwa ndivyo, itakuwa ni kama kupitia moto.”c—1 Wakorintho 3:14, 15.
14. (a) Huenda wafanya-wanafunzi Wakristo ‘wakapataje hasara,’ hata hivyo huenda wao wakafikiaje wokovu kama kupitia moto? (b) Tunaweza kupunguzaje hatari ya kupata hasara?
14 Ni maneno yenye kuamsha fikira kama nini! Inaweza kuumiza sana kujitahidi kusaidia mtu awe mwanafunzi, kisha kumwona huyo mtu akishindwa na jaribu au mnyanyaso na hatimaye kuacha ile kweli. Paulo anakubaliana na jambo hilo anaposema kwamba sisi hupata hasara katika visa kama hivyo. Jambo hilo linaweza kuwa lenye kuumiza sana hivi kwamba wokovu wetu unafafanuliwa kuwa ‘kama unapitia moto’—kama mtu aliyepoteza kila kitu motoni, naye mwenyewe akaponea chupuchupu. Tunaweza kupunguzaje hatari ya kupata hasara upande wetu? Jenga kwa vifaa vidumuvyo! Tukiwafundisha wanafunzi wetu ili kuwafikia mioyo, tukiwachochea wathamini sifa za Kikristo kama vile hekima, ufahamu, kumhofu Yehova, na imani ya kweli, basi tunajenga kwa vifaa vyenye kudumu, visivyoweza kushika moto. (Zaburi 19:9, 10; Mithali 3:13-15; 1 Petro 1:6, 7) Wanaojipatia sifa hizo wataendelea kufanya mapenzi ya Mungu; nao wana tumaini hakika la kuendelea kuwa hai milele. (1 Yohana 2:17)
-