Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoa Ushahidi kwa Watu wa Lugha na Dini Zote
    Huduma ya Ufalme—1998 | Februari
    • 21 Kutoa Ushahidi kwa Wahindu: (Ona sura ya 5 katika kitabu Jitihada ya Ainabinadamu ya Kutafuta Mungu.) Uhindu hauna kanuni za imani hususa. Falsafa yake ni tata sana. Wahindu wana dhana ya utatu ya mungu wao mkubwa Brahman (Brahma aliye Muumba, Vishnu aliye Mhifadhi, na Siva aliye Mwangamizi). Itikadi ya nafsi isiyoweza kufa ni muhimu kwa fundisho lao la kuzaliwa upya katika umbo jingine, ambalo huelekea kuwapa Wahindu maoni ya maisha kuwa ni majaliwa tu. (Ona kitabu Kutoa Sababu, ukurasa wa 154-158, na Mnara wa Mlinzi, Mei 15, 1997, ukurasa wa 3-8.) Uhindu hufunza uvumilivu, kwamba dini zote zaongoza kwenye kweli ileile.

      22 Mfikio upaswao kuchukuliwa ili kutolea Mhindu ushahidi ni kueleza tumaini letu linalotegemea Biblia la kuishi milele tukiwa binadamu wakamilifu duniani na vilevile majibu yenye kuridhisha ambayo Biblia hutoa kwa maswali ya maana wanayokabili wanadamu wote.

  • Kutoa Ushahidi kwa Watu wa Lugha na Dini Zote
    Huduma ya Ufalme—1998 | Februari
    • Wahindu

      From Kurukshetra to Armageddon—And Your Survival (Kijitabu)

      Our Problems—Who Will Help Us Solve Them? (Broshua)

      The Path of Divine Truth Leading to Liberation (Kijitabu)

      Victory Over Death—Is It Possible for You? (Kijitabu)

      Why Should We Worship God in Love and Truth? (Broshua)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki