Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Rashi Mfafanuzi wa Biblia Mwenye Uvutano Mkubwa
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • Kwa kuongezea, kwa karne nyingi mwelekeo wenye nguvu katika Dini ya Kiyahudi ya kirabi ulivunja watu moyo wasichunguze maana halisi ya maandishi ya Kibiblia. Mafafanuzi yasiyo dhahiri na hekaya zilizohusu maneno na mistari ya Kibiblia zilikuwa nyingi. Mengi ya mafafanuzi hayo na hekaya zilirekodiwa katika mabuku makubwa, ambayo kwa ujumla huitwa Midrash.b

  • Rashi Mfafanuzi wa Biblia Mwenye Uvutano Mkubwa
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • b Neno “Midrash” hutokana na mzizi wa neno la Kiebrania linalomaanisha “kuuliza, kujifunza, kuchunguza,” na kwa maana pana zaidi, “kuhubiri.”

  • Rashi Mfafanuzi wa Biblia Mwenye Uvutano Mkubwa
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • Lakini fasihi ya Kimidrash iliyokuwa nyingi mno, ambayo Wayahudi waliijua vizuri sana, haingeweza kupuuzwa. Sehemu yenye kutokeza ya kitabu cha ufafanuzi cha Rashi ni njia ambayo yeye hufafanua yale maandishi ya Kimidrash ambayo mara nyingi yalificha maana halisi ya maandiko ya Biblia.

      Katika ufafanuzi wake wa andiko la Mwanzo 3:8, Rashi aeleza: “Kuna midrashim, yenye masimulizi mengi (aggadicc) ambayo Watu wetu Wenye Hekima tayari wamepanga ifaavyo katika diwani ya Bereshit Rabbah na diwani nyingine za Kimidrash. Hata hivyo, mimi ninapendezwa tu na maana iliyo wazi (peshat) ya mstari, na zile aggadot, (yaani masimulizi), zenye kufafanua simulizi la Kimaandiko katika muktadha wake.” Kwa kuteua na kuhariri midrash ile tu ambayo kulingana na maoni yake ilisaidia kubainisha maana au muktadha wa mstari, Rashi aliondoa, au kutoa, midrash iliyosababisha upingamizi na utatanishi. Tokeo la uhariri huo likawa kwamba vizazi vya baadaye vya Wayahudi vilikuja kufahamiana hasa na sehemu bora kabisa za Midrash ambazo ziliteuliwa na Rashi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki