Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Mungu Awarehemu Mabaki
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • ‘Chipukizi la Yehova’

      5, 6. (a) Isaya aufafanuaje wakati wenye amani baada ya tufani inayokuja? (b) Ni nini maana ya neno “chipukizi,” nalo laonyesha nini juu ya nchi ya Yuda?

      5 Sauti ya Isaya yachangamka atazamapo mbele kwenye kipindi cha amani baada ya tufani inayokuja. Aandika: “Siku hiyo chipukizi la BWANA [“Yehova,” “NW”] litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.”—Isaya 4:2.

      6 Hapo Isaya azungumza juu ya urudisho. Neno la Kiebrania linalofasiriwa “chipukizi” larejezea ‘kile kinachoanza kuchipuka, mche, tawi.’ Hilo huhusianishwa na ufanisi, ongezeko, na baraka kutoka kwa Yehova. Kwa hiyo Isaya atoa wazo la tumaini—ukiwa unaokuja hautadumu milele. Kwa baraka ya Yehova, nchi ya Yuda iliyokuwa imesitawi hapo awali itazaa tena matunda mengi.a—Mambo ya Walawi 26:3-5.

      7. Chipukizi la Yehova litakuwaje “zuri, lenye utukufu”?

      7 Isaya atumia maneno dhahiri kufafanua utukufu wa mabadiliko yaliyo mbele. Chipukizi la Yehova “litakuwa zuri, lenye utukufu.” Neno “zuri” latukumbusha juu ya uzuri wa Bara Lililoahidiwa wakati ambapo Yehova aliwapa Israeli bara hilo karne kadhaa mapema. Lilikuwa zuri sana hivi kwamba lilionwa kuwa “utukufu [“kito,” New American Bible] wa nchi zote.” (Ezekieli 20:6) Hivyo, maneno ya Isaya yawahakikishia watu hao kuwa nchi ya Yuda itarudishwa kwenye utukufu na uzuri wake wa hapo awali. Kwa kweli, itakuwa kama kito kitukufu duniani.

      8. Ni nani watakaokuwapo ili kufurahia uzuri uliorudishwa wa nchi, na Isaya aelezaje hisia zao?

      8 Japo hivyo, ni nani watakaokuwapo ili kufurahia uzuri uliorudishwa wa nchi hiyo? “Waisraeli wale waliookoka,” aandika Isaya. Naam, baadhi ya watu wataokoka uharibifu wenye kufedhehesha uliotabiriwa hapo awali. (Isaya 3:25, 26) Mabaki ya wenye kuokoka watarudi Yuda nao watashiriki kuirudisha. Kwa hao waliorudishwa—“walioponyoka”—mazao mengi ya nchi yao iliyorudishwa “yatakuwa mema sana, na kupendeza.” (Isaya 4:2; NW, kielezi-chini) Fedheha iliyoletwa na ukiwa itabadilika na kuwa hali mpya ya kujionea fahari.

      9. (a) Maneno ya Isaya yalitimizwaje mwaka wa 537 K.W.K.? (b) Kwa nini yaweza kusemwa kuwa “walioponyoka” hutia ndani baadhi ya wale waliozaliwa uhamishoni? (Ona kielezi-chini.)

      9 Kupatana na maneno ya Isaya, dhoruba ya hukumu ilifika mwaka wa 607 K.W.K. Wababiloni walipoharibu Yerusalemu na Waisraeli wengi wakaangamia. Baadhi yao waliokoka na kupelekwa uhamishoni huko Babiloni, lakini isingekuwa kwa sababu ya rehema ya Mungu, hakuna yeyote ambaye angeokoka. (Nehemia 9:31) Hatimaye, Yuda iliachwa ukiwa kabisa. (2 Mambo ya Nyakati 36:17-21) Ndipo, mwaka wa 537 K.W.K., Mungu wa rehema akawaruhusu “walioponyoka” warejee Yuda ili kuirudisha ibada ya kweli.b (Ezra 1:1-4; 2:1) Toba ya dhati ya wahamishwa hao waliokuwa wakirudi yasimuliwa vema katika Zaburi 137, ambayo labda iliandikiwa utekwani au muda mfupi baadaye. Waliporudi Yuda, walilima na kupanda mbegu nchini humo. Hebu wazia jinsi ambavyo hapana budi walihisi walipoona kwamba Mungu anabariki juhudi zao, akiifanya nchi kuchipuka kama “bustani ya Edeni” yenye kuzaa sana!— Ezekieli 36:34-36, BHN.

  • Yehova Mungu Awarehemu Mabaki
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • b “Walioponyoka” walitia ndani baadhi ya wale waliozaliwa uhamishoni. Hao wangeonwa kuwa ‘wameponyoka,’ kwa maana hawangalizaliwa kamwe ikiwa babu zao hawangaliokoka uharibifu.—Ezra 9:13-15; linganisha Waebrania 7:9, 10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki