-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
18. Wale ambao wamemwacha Yehova watabaki na kitu gani, na kuapa kwa jina lao huenda kukawa kunadokeza nini?
18 Yehova anaendelea kuongea na wale ambao wamemwacha: “Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine. Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.” (Isaya 65:15, 16) Wale ambao wamemwacha Yehova watabaki na jina lao tu, nalo litatumika katika kuapa tu, au kulaani. Huenda hiyo ikamaanisha kwamba wale wanaotaka kujifunga kwa kiapo kizito, watakuwa ni kama wanasema hivi: ‘Nisipotimiza ahadi hii, acha nipatwe na adhabu iliyowapata wale waasi-imani.’ Huenda hata ikamaanisha kwamba jina lao litatumiwa kwa njia ya mfano, kama Sodoma na Gomora, ili liwe mfano wa adhabu ya Mungu juu ya waovu.
19. Watumishi wa Mungu wataitwaje jina jingine, na kwa nini watakuwa na uhakika wa kumwamini yule Mungu wa uaminifu? (Ona pia kielezi-chini.)
19 Lakini hali ya watumishi wa Mungu itakuwa tofauti kama nini! Wataitwa jina jingine. Hiyo ni kuonyesha kwamba watabarikiwa na kuheshimiwa wakiisha kurudi katika nchi ya kwao. Hawatatafuta baraka kwa mungu yeyote wa uwongo wala hawataapa kwa jina la sanamu yoyote isiyo na uhai. Bali, wanapojibariki au kuapa, watafanya hivyo kwa jina la yule Mungu wa uaminifu. (Isaya 65:16, kielezi-chini katika tafsiri ya NW) Wakaaji wa nchi watakuwa na sababu ya kumwamini Mungu wakiwa na uhakika kabisa, kwani atakuwa amethibitisha kuwa yeye ni mtimizaji wa ahadi zake.c Wayahudi wakiisha kuwa salama nchini mwao, wataisahau upesi misononeko iliyowapata zamani.
“Ninaumba Mbingu Mpya na Dunia Mpya”
20. Ahadi ya Yehova ya “mbingu mpya na dunia mpya” ilitimizwaje mwaka wa 537 K.W.K.?
20 Sasa Yehova anaieleza kwa mapana na marefu ahadi yake ya kuwarudishia hali nzuri wale mabaki wenye toba wakiisha kurejea kutoka uhamishoni Babiloni. Kupitia Isaya, Yehova anasema hivi: “Tazama, mimi ninaumba mbingu mpya na dunia mpya, na maneno ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.” (Isaya 65:17, “Zaire Swahili Bible”) Ni hakika kwamba ahadi ya Yehova ya kurudishwa kwa hali za kwanza itatimizwa, kwa hiyo yeye anaongea kana kwamba tukio hilo la wakati ujao la kurudishwa kwa hali za kwanza limekwisha anza. Unabii huu ulitimizwa mara ya kwanza mwaka wa 537 K.W.K. wakati mabaki Wayahudi waliporudishwa Yerusalemu. “Mbingu mpya” zilikuwa nini wakati huo? Zilikuwa ugavana wa Zerubabeli ulioungwa mkono na Kuhani wa Cheo cha Juu, Yoshua, mahali pakuu pa ugavana huo pakiwa ni Yerusalemu. Mabaki Wayahudi waliorudishwa ndio waliokuwa “dunia mpya,” yaani jamii iliyosafishwa, nao walijitiisha chini ya utawala huo na kusaidia kuanzisha upya ibada safi nchini. (Ezra 5:1, 2) Shangwe ya kurudishwa huko ilifunika mateso yote ya zamani; misononeko ya zamani hata haikukumbukwa.—Zaburi 126:1, 2.
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
“Tazama, Watumishi Wangu Watafurahi”
16. Yehova atawabariki watumishi wake waaminifu kwa njia zipi, lakini itakuwaje kwa wale ambao wamemwacha?
16 Unabii unaeleza kwamba kuna thawabu tofauti-tofauti ambazo zinawangoja wale wanaomwabudu Mungu kwa moyo mweupe na wale wanaofanya hivyo kwa unafiki. Unafanya hivyo kwa kuwakaripia wale ambao wamemwacha Yehova: “Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha [“hali njema,” “NW”] ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu.” (Isaya 65:13, 14) Yehova atawabariki watumishi wake waaminifu. Wakiwa na mioyo inayofurika shangwe, watabubujika kelele za furaha. Kula, kunywa, na kufurahi ni maneno yanayoonyesha kwamba Yehova atatosheleza mahitaji ya waabudu wake kwa vitu kemkemu. Tofauti na hivyo, wale ambao wamechagua kumwacha Yehova wataona njaa na kiu ya kiroho. Mahitaji yao hayatatoshelezwa. Watalia kwa sauti kubwa na kupiga makelele ya kuomboleza kwa uchungu na msononeko.
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
24. Kwa nini Yehova atashangilia kurudishwa kwa Yerusalemu, na ni nini ambacho hakitasikiwa tena katika barabara za jiji?
24 Unabii wa Isaya unaendelea kusema hivi: “Furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.” (Isaya 65:18, 19) Si Wayahudi peke yao watakaoshangilia kurudishwa kwenye nchi yao, bali Mungu mwenyewe atashangilia pia, kwa maana atarembesha jiji la Yerusalemu—ambalo kwa mara nyingine litakuwa limekuwa mahali pakuu pa ibada ya kweli duniani. Ile sauti ya kulia kwa sababu ya maafa, iliyosikiwa katika barabara za jiji miongo kadhaa mapema, haitasikiwa tena.
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Ahadi ya Wakati Ujao Wenye Usalama
27. Isaya anaelezaje kuhusu usalama ambao wale wenye kurudi wataufurahia katika nchi yao?
27 Katika utimizo wa kwanza, maisha yatakuwaje kwa Wayahudi wenye kurudi wakiwa chini ya mbingu mpya? Yehova anasema hivi: “Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.” (Isaya 65:20) Hiyo inaonyesha vizuri kama nini usalama ambao wahamishwa wenye kurudi watafurahia katika nchi yao iliyorudishwa! Kifo kisichotazamiwa hakitampata mzaliwa-juzi, maana yake kitoto cha siku chache tu. Wala kifo cha jinsi hiyo hakitammaliza mzee asiyetimiza maisha yake.d Maneno ya Isaya yanawafariji kweli kweli Wayahudi watakaorudi Yuda! Wakiisha kuwa salama nchini mwao, hawana tena haja ya kufanya wasiwasi eti adui zao watasomba watoto wao wachanga au kuchinja mashujaa wao.
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
29. (a) Watu wa Mungu walio watiifu watapata shangwe zipi katika nchi ya Yuda iliyorudishwa? (b) Kwa nini miti ni mfano unaofaa wa maisha marefu? (Ona kielezi-chini.)
29 Yehova anaendelea kueleza juu ya hali zitakazokuwako katika nchi iliyorudishwa ya Yuda: “Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.” (Isaya 65:21, 22) Baada ya kuirudia nchi ya Yuda, ambayo bila shaka haikuwa na nyumba wala mizabibu, watu wa Mungu walio watiifu watakuwa na shangwe ya kuishi katika nyumba zao wenyewe na kula matunda kutoka mashamba yao wenyewe ya mizabibu. Mungu ataibariki kazi yao, na wataishi maisha marefu—marefu kama siku za mti—wafurahie matunda ya kazi zao.e
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
33. Wayahudi watakapoirudia nchi yao, wanyama wataishije kwa amani?
33 Amani na usalama ambazo zimeahidiwa zitakuwa za kiasi gani? Yehova anamalizia sehemu hii ya unabii kwa kusema hivi: “Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema BWANA.” (Isaya 65:25) Wakati mabaki ya Wayahudi waaminifu watakapoirudia nchi yao, watakuwa chini ya utunzaji wa Yehova. Itakuwa ni kama simba anakula majani kama ng’ombe, kwa maana simba hatawadhuru Wayahudi wala wanyama wao wa kufugwa. Ahadi hiyo ni hakika, kwa maana inamalizika kwa kusema, ‘asema Yehova.’ Na neno lake hutimia daima!—Isaya 55:10, 11.
-