Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu ‘Aimarisha Haki Duniani’
    Mkaribie Yehova
    • 1, 2. Yesu alikasirika pindi gani, na kwa nini?

      YESU alikuwa amekasirika sana, na kwa sababu nzuri. Huenda ikawa vigumu kuwazia kwamba Yesu ambaye alikuwa mpole sana angeweza kukasirika. (Mathayo 21:5) Bila shaka alijidhibiti kikamili kwa kuwa hasira yake ilikuwa adilifu.a Lakini ni nini kilichomkasirisha mwanamume huyo aliyependa amani? Alikasirishwa na ukosefu mbaya wa haki.

      2 Yesu alipenda mno hekalu la Yerusalemu. Lilikuwa ndilo jengo pekee takatifu ulimwenguni pote lililowekwa wakfu kwa ajili ya ibada ya Baba yake wa mbinguni. Wayahudi walisafiri kutoka nchi nyingi za mbali ili kuabudu huko. Hata watu wasio Wayahudi ambao walimcha Mungu walikuja katika ua wa hekalu uliotengwa kwa ajili yao. Lakini mapema katika huduma yake, Yesu aliingia hekaluni na kuona hali yenye kusikitisha sana. Hekalu lilikuwa kama soko badala ya kuwa nyumba ya ibada! Umati mkubwa wa wafanyabiashara na wavunja-fedha ulijaa hekaluni. Lakini kulikuwaje na ukosefu wa haki? Watu hao waliona hekalu la Mungu kuwa mahali pa kuwalaghai watu—hata kuwaibia. Jinsi gani?—Yohana 2:14.

      3, 4. Ni ulaghai gani wa pupa ulioendelea katika nyumba ya Yehova, na Yesu alichukua hatua gani kuukomesha?

      3 Viongozi wa kidini walikuwa wameamua kwamba ni aina moja tu ya sarafu ingeweza kutumiwa kulipa kodi ya hekalu. Wageni walilazimika kuvunja fedha zao ili kupata sarafu hizo. Kwa hiyo, wavunja-fedha walifanyia kazi yao hekaluni, na walitoza malipo fulani kwa ajili ya kuvunja fedha. Biashara ya kuuza wanyama ilileta faida kubwa pia. Wageni waliotaka kutoa dhabihu wangeweza kununua wanyama kutoka kwa mfanyabiashara yeyote mjini, lakini huenda wakuu wa hekalu wangekataa dhabihu hizo eti hazifai. Lakini, walikubali mara moja wanyama wa dhabihu walionunuliwa hekaluni. Nyakati nyingine watu hao wasio na uwezo waliuziwa wanyama kwa bei ghali sana.b Biashara hiyo ilikuwa mbaya kuliko ulaghai. Ulikuwa unyang’anyi!

      “Ondoleeni mbali vitu hivi kutoka hapa!”

      4 Yesu hakuweza kuvumilia ukosefu huo wa haki. Hiyo ilikuwa nyumba ya Baba yake! Alisokota mjeledi wa kamba akafukuza makundi ya ng’ombe na kondoo kutoka hekaluni. Kisha akazipindua meza za wavunja-fedha. Hebu wazia jinsi sarafu hizo zote zilivyobingirika kotekote kwenye sakafu ya marumaru! Akawaamuru hivi kwa ukali wale wauza-njiwa: “Ondoleeni mbali vitu hivi kutoka hapa!” (Yohana 2:15, 16) Yaonekana hakuna yeyote aliyethubutu kumpinga mwanamume huyo jasiri.

  • Yesu ‘Aimarisha Haki Duniani’
    Mkaribie Yehova
    • b Mishnah inasema kwamba miaka kadhaa baadaye watu walilalamika kwa sababu njiwa waliuzwa kwa bei ghali sana hekaluni. Kisha bei ikapunguzwa mara moja kwa asilimia 99! Ni nani waliopata faida kubwa kutokana na biashara hiyo yenye ufanisi? Wanahistoria fulani wanadokeza kwamba masoko ya hekaluni yalimilikiwa na jamaa ya Anasi yule Kuhani wa Cheo cha Juu. Jamaa hiyo ya kikuhani ilipata ufanisi mkubwa sana kutokana na masoko hayo.—Yohana 18:13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki