Biblia Ilisema Hivyo Kwanza
● “Maongezi hayakuanza kamwe mara moja, wala hayakuwa ya haraka haraka. Hakuna yeyote aliyefanya upesi kuuliza swali, hata liwe muhimu namna gani, na hakuna yeyote aliyeshurutishwa kujibu. Kutua ili mtu aweze kufikiria kulikuwa njia yenye adabu sana ya kuanza na kuendeleza maongezi. Kukaa kimya kulikuwa muhimu sana kwa watu wa Lakota . . . [Hili] lilifanywa ili kuonyesha heshima ya kweli na staha kwa ile sheria iliyosema, ‘fikiri kwanza kabla hujasema.’”—Luther Standing Bear, kiongozi wa kabila la Oglala Sioux (1868?-1939).
“Jueni hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mtu lazima awe mwepesi sana juu ya kusikia, wa polepole juu ya kusema, wa polepole juu ya hasira ya kisasi.”—Yakobo 1:19, Biblia (karne ya kwanza K.W.K.).
“Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu, bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.”—Mithali 15:28, Biblia (karibu karne ya nane K.W.K.).
“Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.”—Mithali 29:11, Biblia (karibu karne ya nane K.W.K.).
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 27]
Photo by David Barry, the Denver Public Library, Western History Collection