Mfululizo wa Matukio
“Hapo mwanzo . . . ”
4026 K.W.K. Kuumbwa kwa Adamu
3096 K.W.K. Kifo cha Adamu
2370 K.W.K. Gharika yaanza
2018 K.W.K. Abrahamu azaliwa
1943 K.W.K. Agano la Kiabrahamu
1750 K.W.K. Yosefu auzwa utumwani
kabla ya 1613 K.W.K. Ayubu ajaribiwa
1513 K.W.K. Kutoka Misri
1473 K.W.K. Taifa la Israeli laingia Kanaani likiongozwa na Yoshua
1467 K.W.K. Ushindi dhidi ya Kanaani wakamilika
1117 K.W.K. Sauli atiwa mafuta awe mfalme
1070 K.W.K. Mungu amwahidi Daudi Ufalme
1037 K.W.K. Sulemani awa mfalme
1027 K.W.K. Hekalu la Yerusalemu lakamilika
mnamo 1020 K.W.K. Wimbo wa Sulemani wakamilika
997 K.W.K. Taifa la Israeli lagawanyika na kuwa falme mbili
mnamo 717 K.W.K. Kuandikwa kwa Methali kwakamilika
607 K.W.K. Jiji la Yerusalemu laharibiwa; uhamisho wa Babiloni waanza
539 K.W.K. Koreshi aangusha Babiloni
537 K.W.K. Wayahudi warudi Yerusalemu
455 K.W.K. Kuta za Yerusalemu zajengwa upya; Majuma 69 ya miaka yaanza
Baada ya 443 K.W.K. Malaki akamilisha kitabu chake cha kinabii
mnamo 2 K.W.K. Kuzaliwa kwa Yesu
29 W.K. Yesu abatizwa Yesu aanza kuhubiri kuhusu Ufalme wa Mungu
31 W.K. Yesu achagua mitume 12; Mahubiri ya Mlimani
32 W.K. Yesu amfufua Lazaro
Nisani 14, 33 W.K. Yesu atundikwa (Sehemu ya mwezi wa 3 na sehemu ya mwezi wa 4 katika kalenda ya leo)
Nisani 16, 33 W.K. Yesu afufuliwa
Sivani 6, 33 W.K. Pentekoste; roho takatifu yamiminwa (Sehemu ya mwezi wa 5 na sehemu ya mwezi wa 6 katika kalenda ya leo)
36 W.K. Kornelio awa Mkristo
mnamo 47-48 W.K. Safari ya kwanza ya Paulo ya kuhubiri
mnamo 49-52 W.K. Safari ya pili ya Paulo ya kuhubiri
mnamo 52-56 W.K. Safari ya tatu ya Paulo ya kuhubiri
mnamo 60-61 W.K. Paulo aandika barua akiwa gerezani Roma
kabla ya 62 W.K. Yakobo, ndugu wa kambo wa Yesu, aandika barua yake
66 W.K. Wayahudi waasi dhidi ya Roma
70 W.K. Waroma waharibu Yerusalemu pamoja na hekalu lake
mnamo 96 W.K. Yohana aandika Ufunuo
mnamo 100 W.K. Kifo cha Yohana, mtume wa mwisho