Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • 9. Ingawa kimsingi Paulo alikuwa mweka-msingi, yeye alikuwa na hangaiko lipi kuhusu wale waliokubali ukweli wa yale aliyofundisha?

      9 Paulo aliandika: “Basi yeyote akijenga juu ya huo msingi, dhahabu, fedha, mawe yenye bei, vifaa vya mbao, nyasi kavu, mabua, kazi ya kila mmoja itakuwa dhahiri, kwa maana ile siku itaifichua, kwa sababu itafunuliwa kwa njia ya moto; na moto wenyewe utathibitisha ni ya namna gani kazi ya kila mmoja.” (1 Wakorintho 3:12, 13) Paulo alimaanisha nini? Fikiria hali ya wakati huo. Kimsingi Paulo alikuwa mweka-msingi. Katika safari zake za umishonari, alisafiri kutoka jiji hadi jiji, akihubiria wengi ambao hawakuwa wamesikia kamwe juu ya Kristo. (Waroma 15:20) Watu walipokubali kweli aliyofundisha, makutaniko yalifanyizwa. Paulo aliwajali sana waaminifu hao. (2 Wakorintho 11:28, 29) Hata hivyo, kazi yake ilimtaka aendelee kusafiri. Kwa hiyo, baada ya kutumia miezi 18 akiweka msingi huko Korintho, aliondoka kwenda kuhubiri katika majiji mengine. Hata hivyo, alipendezwa sana na jinsi wengine walivyoendeleza kazi aliyokuwa amefanya huko.—Matendo 18:8-11; 1 Wakorintho 3:6.

  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • 11 Ni nini ambacho kingeyapata majengo hayo yakishika moto? Jibu lilikuwa wazi siku ya Paulo kama lilivyo siku yetu. Kwa kweli, huko nyuma mwaka wa 146 K.W.K., jiji la Korintho lilikuwa limeshindwa na kuwashwa moto na Jenerali Mummius wa Roma. Kwa kweli, majengo mengi ya mbao, nyasi kavu, au bua yaliharibiwa kabisa. Vipi majengo imara ya mawe yaliyokuwa yamepambwa kwa fedha na dhahabu? Hapana shaka haya yaliokoka. Huenda ikawa wanafunzi wa Paulo huko Korintho walipitia karibu na majengo hayo kila siku—majengo ya mawe yenye fahari yaliyookoka misiba ambayo zamani ilikuwa imeharibu majengo ya muda yaliyokuwa karibu. Paulo alidhihirisha hoja yake kwa mkazo ulioje! Tunapofundisha twahitaji kujiona kuwa wajenzi. Twataka kutumia vifaa bora zaidi na vyenye kudumu zaidi iwezekanavyo. Kwa njia hiyo, yaelekea zaidi kwamba kazi yetu itadumu. Vifaa hivyo vyenye kudumu ni vipi, na kwa nini ni muhimu kuvitumia?

  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • 12. Wakristo Wakorintho walikuwa wakifanyaje kiholela kazi ya kujenga?

      12 Kwa wazi, Paulo alihisi kwamba Wakristo katika Korintho walikuwa wakijenga vibaya. Kasoro ilikuwa nini? Kama vile muktadha uonyeshavyo, kutaniko hilo lilikuwa limekumbwa na mgawanyiko, kuvutiwa na watu mashuhuri kujapohatarisha umoja wa kutaniko. Baadhi yao walikuwa wakisema, “Mimi ni wa Paulo,” ilhali wengine walisisitiza, “Mimi ni wa Apolo.” Yaonekana wengine walijivunia mno hekima yao wenyewe. Si ajabu kwamba matokeo yalikuwa hali ya kufikiri kimwili, kutokomaa kiroho, na “wivu na zogo” iliyoenea sana. (1 Wakorintho 1:12; 3:1-4, 18) Bila shaka mitazamo hiyo ilidhihirika katika mafundisho yaliyofanywa kutanikoni na hudumani. Matokeo yalikuwa kwamba kazi yao ya kufanya wanafunzi ilifanywa kiholela, kama kazi ya kujenga iliyofanywa kwa vifaa duni. Haingeokoka “moto.” Paulo alikuwa akizungumzia moto upi?

      13. Moto katika kielezi cha Paulo wawakilisha nini, na yawapasa Wakristo wote wajue nini?

      13 Kuna moto ambao sisi sote hukabili maishani—majaribu ya imani yetu. (Yohana 15:20; Yakobo 1:2, 3) Kama vile tunavyohitaji kujua leo, Wakristo katika Korintho walihitaji kujua kwamba kila mtu tunayefundisha kweli atajaribiwa. Tukifundisha vibaya, huenda matokeo yakawa yenye kusikitisha. Paulo alionya: “Kazi ya yeyote ambayo ameijenga juu ya huo ikibaki, atapokea thawabu; kazi ya yeyote ikichomwa kabisa, atapata hasara, lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini, ikiwa ndivyo, itakuwa ni kama kupitia moto.”c—1 Wakorintho 3:14, 15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki