-
‘Kufahamu Sisi Ni Nini Wakati wa Ukumbusho’Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
-
-
3 “Bwana Yesu katika usiku ambamo yeye alikuwa akienda kutolewa alichukua mkate na, baada ya kutoa shukrani, akauvunja na kusema: ‘Huu humaanisha mwili wangu ambao ni kwa ajili yenu. Fulizeni kufanya hivi kwa kukumbuka mimi.’ Alifanya hivyo hivyo kwa habari ya kikombe pia, baada ya yeye kwisha kuwa na mlo wa jioni, akisema: ‘Kikombe hiki humaanisha agano jipya kwa nguvu za damu yangu. Fulizeni kufanya hivi, mara nyingi nyinyi mnapokinywa, kwa kukumbuka mimi.’ Kwa maana mara nyingi nyinyi mnapokula mkate huu na mnapokunywa kikombe hiki, mwafuliza kupiga mbiu juu ya kifo cha Bwana, mpaka yeye awasili.”—1 Wakorintho 11:23-26, NWa

Divai Yenye Maana
9. Ni mfano gani mwingine ambao Yesu alisema wapasa kutumiwa?
9 Yesu alitumia kifananisho kingine: “Pia alichukua kikombe, na baada ya kushukuru Mungu akakitoa kwao akisema, ‘Nyweni yacho, nyinyi nyote; hii yamaanisha damu yangu, damu-agano mpya, yenye kudondoshwa kwa ajili ya wengi, ili wapate ondoleo la madhambi yao.’” (Mathayo 26:27, 28, Moffatt) Ni nini kilichokuwa katika hicho kikombe cha ushirika alichokipitisha, nacho chamaanisha nini kwetu wakati tujitahidipo kufahamu sisi wenyewe ni nini?
10. Divai ilipataje nafasi katika Sikukuu-Kupitwa ya Kiyahudi?
10 Musa alipofanya mpangilio wa karamu ya Sikukuu-Kupitwa hapo kwanza, hakutaja kinywaji chochote. Wanachuo wengi huitikadi kwamba divai ilianzishwa katika Sikukuu-Kupitwa muda mwingi baadaye, labda katika karne ya pili K.W.K.b Vyovyote vile, ilikuwa kawaida kutumia divai katika mlo huu katika karne ya kwanza, na Yesu hakuikataa. Aliitumia divai ya Sikukuu-Kupitwa alipokuwa akianzisha Ukumbusho.
11. Ni divai ya namna gani ambayo yafaa kutumiwa wakati wa Mlo wa Jioni wa Bwana?
11 Kwa kuwa Sikukuu-Kupitwa ya Kiyahudi ilitukia muda mrefu baada ya mavuno ya mzabibu, Yesu angalikuwa akitumia, si maji-matunda yasiyochachwa, bali divai nyekundu ambayo ingeweza kwa urahisi kuwakilisha damu yake. (Linganisha Ufunuo 14:20.) Damu ya Kristo haikuhitaji kuongezewa kitu, kwa hiyo divai isiyokolezwa kitu yafaa, badala ya divai zenye kutiwa ukali wa brandi (kama vile port, sherry, au muscatel) au zenye vikolezo au mimea-teketeke vikiwa vimeongezwa (vermouth, Dubonnet, au nyingi za divai za kuamsha hamu ya kula). Ingawa hivyo, sisi hatuhitaji kuwa na wasiwasi divai ilitayarishwaje, kama kiasi fulani cha sukari kiliongezwa wakati wa kuichachisha ili iwe na ladha ya wastani au yenye kileo au kama salfa kidogo ilitumiwa kuizuia isiharibike.c Makundi mengi hutumia divai nyekundu ya kibiashara (kama vile Chianti, Burgundy, Beaujolais, au claret) au divai nyekundu iliyofanyizwa nyumbani. Divai na mkate huwa ni mifano tu, au vifananisho; kwa sababu hiyo, yoyote ambayo haikutumiwa yaweza kupelekwa nyumbani itumiwe baadaye kama chakula kinginecho au vinywaji.
12. Yesu alieleza kwamba divai ina maana gani ya uwakilishi?
12 Uhakika wa kwamba Yesu alinena juu ya damu yake katika usiku wa Sikukuu-Kupitwa ungaliweza kukumbusha juu ya damu ya mwana-kondoo huko nyuma katika Misri. Lakini angalia jinsi Yesu alivyofanya ulinganisho tofauti, akisema: “Kikombe hiki humaanisha agano jipya kwa nguvu za damu yangu ipasayo kumwagwa kwa ajili yenu.” (Luka 22:20, NW) Mapema kidogo Mungu alikuwa amefanyiza agano pamoja na taifa la Israeli wa kimnofu, nalo lilianzishwa kwa damu ya dhabihu za wanyama. Kulikuwako ulinganifu kati ya damu ya dhabihu hizo na damu ya Yesu. Zote mbili zilihusika katika kuanzisha kwa Mungu agano pamoja na taifa la watu wake. (Kutoka 24:3-8; Waebrania 9:17-20) Sehemu moja ya agano la Sheria ilikuwa kwamba Israeli wa kimnofu walikuwa na tazamio la kujumlika kuwa taifa la wafalme-makuhani. (Kutoka 19:5, 6) Hata hivyo, baada ya Israeli kushindwa kushika agano la Yehova, yeye alisema kwamba angeweka “agano jipya” mahali pa “lile la hapo kwanza.” (Waebrania 9:1, 15; Yeremia 31:31-34, NW) Kikombe cha divai ambacho sasa Yesu alipitisha miongoni mwa mitume wenye imani kiliwakilisha agano jipya hili.
-
-
‘Kufahamu Sisi Ni Nini Wakati wa Ukumbusho’Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
-
-
a “Katika usiku ambao Yeye alitolewa, Bwana Yesu alichukua mkate; akitoa shukrani, Yeye akauvunja na kusema: ‘Huu ni mwili wangu ambao ni kwa ajili ya nyinyi; fanyeni hivi kuwa ukumbusho wangu.’ Vivyo hivyo Yeye alichukua kikombe wakati chajio kilipokwisha, akasema: ‘Kikombe hiki ndilo agano jipya, lenye kutiwa muhuri kwa damu yangu; kila wakati mkinywapo, fanyeni hivyo kuwa ukumbusho wangu.’”—An Expanded Paraphrase of the Epistles of Paul, ya F. F. Bruce.
-