-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
1. Mmoja wa malaika saba anafunulia Yohana nini?
KASIRANI ya Yehova ya uadilifu lazima imiminwe mpaka utimilifu, mabakuli saba yayo! Malaika wa sita alipomimina bakuli lake katika kata ya Babuloni wa kale, ilifananisha kwa kufaa tauni kwa Babuloni Mkubwa huku matukio yakienda kasi kuelekea vita ya mwisho kabisa ya Har–Magedoni. (Ufunuo 16:1, 12, 16) Yaelekea, malaika uyu huyu ndiye anayefunua sasa ni kwa nini na jinsi gani Yehova anatekeleza hukumu zake za uadilifu. Yohana anapatwa na mshangao kwa sababu ya anachofuata kusikia na kuona: “Na mmoja wa wale malaika saba ambao walikuwa na mabakuli saba akaja na kunena na mimi, kusema: ‘Njoo, mimi nitaonyesha wewe hukumu juu ya kahaba mkubwa ambaye huketi juu ya maji mengi, ambaye wafalme wa dunia walifanya uasherati na yeye, huku wale ambao huikaa dunia walifanywa kulewa divai ya uasherati wake.’”—Ufunuo 17:1, 2, NW.
2. Kuna ithibati gani kwamba “kahaba mkubwa” (a) si Roma ya kale? (b) si biashara kubwa-kubwa? (c) ni dini?
2 “Kahaba mkubwa”! Kwa nini jina lenye kugutusha hivyo? Yeye ni nani? Wengine wametambulisha kahaba huyu wa ufananisho kuwa Roma ya kale. Lakini Roma ilikuwa mamlaka ya kisiasa. Kahaba huyu hufanya uasherati na wafalme wa dunia, kwa wazi kutia ndani wafalme wa Roma. Mbali na hilo, baada ya kuharibiwa kwake, “wafalme wa dunia,” husemekana kuombolezea kufa kwake. Hivyo, yeye hawezi kuwa mamlaka ya kisiasa. (Ufunuo 18:9, 10) Kwa kuongezea, kwa kuwa anaombolezewa pia na wafanya biashara wa ulimwengu, yeye hawezi kufananisha biashara kubwa-kubwa. (Ufunuo 18:15, 16) Hata hivyo, sisi tunasoma kwamba, ‘kwa mazoea yake ya uwasiliano na roho mataifa yote yaliongozwa vibaya.’ (Ufunuo 18:23, NW) Hilo linafanya iwe wazi kwamba huyu kahaba mkubwa lazima awe dini ya ulimwenguni pote.
3. (a) Kwa nini kahaba mkubwa lazima afananishe zaidi ya Kanisa Katoliki la Roma, au hata Jumuiya ya Wakristo yote? (b) Ni mafundisho gani ya Kibabuloni yanayopatikana katika dini nyingi za Mashariki na pia katika mafarakano ya Jumuiya ya Wakristo? (c) John Henry Newman kardinali Mkatoliki alikiri nini juu ya asili ya mafundisho, sherehe na mazoea mengi ya Jumuiya ya Wakristo? (Ona kielezi cha chini.)
3 Dini ipi? Je! yeye ni Kanisa Katoliki la Roma, kama vile wengine wameshikilia? Au je! yeye ni Jumuiya ya Wakristo yote? Hapana, lazima yeye awe mpana hata zaidi ya hizi ikiwa yeye ataongoza vibaya mataifa yote. Kwa hakika yeye ni milki ya ulimwengu mzima wote ya dini bandia. Chanzo chake katika mafumbo ya Babuloni huonyeshwa kwa njia ya kwamba mengi ya mafundisho na mazoea ya Kibabuloni ni mambo ya kawaida ya dini nyingi kotekote duniani. Mathalani, itikadi ya kwamba nafsi ya kibinadamu ina kutokufa, moto wa mateso, na utatu wa miungu itapatikana katika dini nyingi za Mashariki pamoja na katika mafarakano ya Jumuiya ya Wakristo. Dini bandia, iliyoanguliwa miaka zaidi ya 4,000 iliyopita katika jiji la kale la Babuloni, imesitawi ikawa dubwana la ki-siku-hizi, ambalo kwa kufaa huitwa, Babuloni Mkubwa.a Ingawa hivyo, sababu gani anaelezwa kwa usemi usiopendeza “kahaba mkubwa”?
4. (a) Ni katika njia zipi Israeli wa kale alifanya uasherati? (b) Ni katika njia gani ya kutokeza Babuloni Mkubwa amefanya uasherati?
4 Babuloni (au Babeli, kumaanisha “Mvurugo”) lilifikia kilele chalo cha ukubwa wakati wa Nebukadneza. Lilikuwa dola la dini-siasa lenye mahekalu na vikanisa zaidi ya elfu moja. Ukuhani walo ulitumia nguvu kubwa. Ingawa muda mrefu tangu hapo Babuloni limeacha kuwa serikali ya ulimwengu, Babuloni Mkubwa wa kidini huendelea kuwapo, na kwa kufuata kigezo cha kale, yeye angali anatafuta kuvuta na kuunda mambo ya kisiasa. Lakini je! Mungu anatoa idhini ya dini kuwa katika siasa? Katika Maandiko ya Kiebrania, Israeli alisemwa kuwa alifanya ukahaba wakati alipojihusisha katika ibada bandia na wakati badala ya kuitibari katika Yehova, alifanya mafungamano na mataifa. (Yeremia 3:6, 8, 9; Ezekieli 16:28-30) Babuloni Mkubwa pia hufanya uasherati. Kwa kutokeza, yeye amefanya lolote analoona linafaa ili kupata uvutano na mamlaka juu ya wafalme wa dunia wenye kutawala.—1 Timotheo 4:1.
5. (a) Viongozi wa kidini hufurahia umashuhuri gani? (b) Kwa nini kutamani umashuhuri wa kilimwengu kunapingana moja kwa moja na maneno ya Yesu Kristo?
5 Leo, mara nyingi viongozi wa kidini hugombea cheo cha juu katika serikali, na katika mabara fulani, wanashiriki katika serikali, hata wakishikilia vyeo katika bunge. Katika 1988 viongozi wa kidini wa Kiprotestanti wawili wenye kujulikana sana waligombea cheo cha rais wa United States. Viongozi katika Babuloni Mkubwa hupenda umashuhuri; foto zao mara nyingi zitaonekana katika nyusipepa za umma wanapofuatana na wanasiasa mashuhuri. Kwa kutofautiana, Yesu aliepuka kujihusisha katika siasa na akasema hivi kwa habari ya wanafunzi wake: “Wao si sehemu ya ulimwengu, kama vile mimi si sehemu ya ulimwengu.”—Yohana 6:15; 17:16, NW; Mathayo 4:8-10; ona pia Yakobo 4:4.
‘Ukahaba’ wa Ki-Siku-Hizi
6, 7. (a) Chama cha Nazi cha Hitla kilipataje mamlaka katika Ujeremani? (b) Itifaki ambayo Vatikani ilifanya pamoja na Ujeremani ya Nazi ilisaidiaje Hitla katika jitihada yake kubwa ya kutawala ulimwengu?
6 Kupitia udukizi wake katika siasa, huyu kahaba mkubwa ameletea aina ya binadamu huzuni isiyoelezeka. Mathalani, fikiria mambo ya hakika yaliyomwezesha Hitla kuinuka kwenye mamlaka katika Ujeremani—mambo ya hakika yenye kuchukiza sana ambayo baadhi ya watu wangependa kuyafuta kutoka katika vitabu vya historia. Katika Mei 1924 Chama cha Nazi kilishikilia viti 32 katika Bunge la Ujeremani. Kufikia Mei 1928 vilikuwa vimepungua vikawa viti 12. Lakini, ule Mshuko Mkubwa wa Thamani ya Pesa ukagharikisha ulimwengu katika 1930; kufuata huo, Wanazi walipata nafuu yenye kutokeza, wakijipatia viti 230 kati ya 608 katika machaguzi ya Ujeremani ya Julai 1932. Hivyo, wakawa chama kikubwa zaidi ya vyote katika Bunge. Upesi baadaye, Franz von Papen, Mheshimiwa Kipapa, aliyekuwa Chansela hapo kwanza, akaja kusaidia Wanazi. Kulingana na wanahistoria, von Papen alikuwa na njozi ya Milki Takatifu ya Kiroma mpya. Muda wake mwenyewe mfupi wa kuwa Chansela ulikuwa umekuwa usiofanikiwa, hivyo sasa yeye alitumainia kujipatia mamlaka kupitia Wanazi. Kufikia Januari 1933, yeye alikuwa amepata uungaji-mkono kwa ajili ya Hitla kutoka kwa wenye viwanda, na kwa njama za hila yeye alihakikisha kwamba Hitla amekuwa Chansela wa Ujeremani katika Januari 30, 1933. Yeye mwenyewe alifanywa makamu wa Chansela na yeye alitumiwa na Hitla apate uungaji-mkono wa sehemu za Kikatoliki za Ujeremani. Kwa muda wa miezi miwili ya kujipatia mamlaka, Hitla alivunja bunge, akapeleka maelfu ya viongozi wapinzani kwenye kambi za mateso, na akaanza kampeni iliyo wazi ya kuwaonea Wayahudi.
7 Katika Julai 20, 1933, upendezi wa Vatikani katika mamlaka iliyokuwa ikiinuka ya Unazi ulionyeshwa wakati Kardinali Pacelli (ambaye baadaye akawa Papa Pius 12) alipotia sahihi itifaki katika Roma kati ya Vatikani na Ujeremani ya Nazi. Von Papen alitia sahihi hati hiyo akiwa mwakilishi wa Hitla, na huko huko Pacelli akampa von Papen medali ya juu ya kipapa ya Msalaba Mtukufu wa Daraja la Pius.b Katika kitabu chake Satan in Top Hat, Tibor Koeves huandika juu ya hili, akitaarifu: “Itifaki ilikuwa ushindi mkubwa kwa ajili ya Hitla. Ilimpa uungaji-mkono wa kwanza wa kiadili aliokuwa amepokea kutoka ulimwengu wa nje, na huo kutoka chimbuko lililokwezwa zaidi sana.” Itifaki hiyo ilitaka Vatikani iondoe uungaji-mkono wayo kutoka kwa Chama cha Kati cha Kikatoliki, na hivyo kuidhinisha “serikali jumla” ya Hitla ya chama kimoja.c Zaidi, sehemu ya 14 yayo ilisema: “Uwekwaji rasmi wa maaskofu wakuu, maaskofu, na wengine kama hao utatolewa baada tu ya gavana, aliyewekwa na Serikali, kuhakikisha kabisa kwamba hakuna shaka lolote kwa habari ya mafikirio ya ujumla ya kisiasa.” Kufikia mwisho wa 1933 (uliotangazwa na Papa Pius 11 kuwa “Mwaka Mtakatifu”), uungaji-mkono wa Vatikani ulikuwa umekuwa umechangia sana jitihada kubwa ya Hitla kwa ajili ya utawala wa ulimwengu.
8, 9. (a) Vatikani na pia Kanisa Katoliki na viongozi wa kidini wayo walitendaje katika kuitikia ukatili wa Nazi? (b) Ni taarifa gani ambayo Maaskofu Wakatoliki wa Ujeremani walitoa mwanzoni mwa Vita ya Ulimwengu 2? (c) Mahusiano ya dini-siasa yamekuwa na matokeo gani?
8 Ingawa mapadri na watawa wa kike wachache waliteta dhidi ya matendo ya ubahaimu ya Hitla—na wakapata mateso kwa kufanya hivyo—Vatikani pamoja na Kanisa Katoliki na jeshi layo la viongozi wa kidini waliunga mkono ukatili wa Nazi ama kwa vitendo au kwa kutoteta, waliuona kuwa kinga dhidi ya kusonga mbele kwa Ukomunisti wa ulimwengu. Akijikalia kitako katika Vatikani, Papa Pius 12 aliachilia Uharibifu Mkubwa wa Wayahudi na unyanyaso wa ukatili juu ya Mashahidi wa Yehova na wengine uendelee bila kuchambuliwa. Ni kinyume kwamba Papa John Paul 2, alipozuru Ujeremani katika Mei 1987, alipaswa kutukuza msimamo wa padri mmoja mwenye moyo mweupe wa kupinga Unazi. Yale maelfu mengine ya viongozi wa kidini wa Ujeremani walikuwa wakifanya nini wakati wa utawala wa kuogofya wa Hitla? Barua moja ya uchungaji iliyotolewa na maaskofu wa Ukatoliki wa Ujeremani katika Septemba 1939 ilipotokea Vita ya Ulimwengu 2, inatoa nuru juu ya jambo hili. Kwa sehemu inasomwa hivi: “Katika saa hii ya kukata maneno sisi twashauri askari-jeshi Wakatoliki kufanya wajibu wao katika utii kwa Fuehrer na kuwa tayari kudhabihu nafsi nzima yao. Sisi tunasihi Waaminifu wajiunge katika sala zenye idili kwamba huu Mwongozo wa Kimungu uweze kupeleka vita hii kwenye ufanisi wenye baraka.”
9 Ubalozi huu wa Katoliki unatoa kielezi cha namna ya ukahaba ambao dini imejitia ndani yao katika miaka zaidi ya 4,000 iliyopita katika kubembeleza Serikali ya kisiasa ili kupata mamlaka na faida. Mahusiano kama hayo ya dini-siasa yamesitawisha vita, minyanyaso, na taabu kwa aina ya binadamu kwa kadiri kubwa mno. Jinsi aina ya binadamu inavyoweza kuwa na furaha kwamba hukumu ya Yehova juu ya huyu kahaba mkubwa imekaribia karibu! Na itekelezwe upesi!
Kuketi Juu ya Maji Mengi
10. Ni “maji mengi” gani ambayo Babuloni Mkubwa hutegemea kuwa himaya, na yanapatwa na nini?
10 Babuloni wa kale aliketi juu ya maji mengi—Mto Eufrati na mifereji mingi. Haya yalikuwa himaya yake pamoja na chimbuko la biashara iliyotokeza utajiri, mpaka yalipokaushwa usiku mmoja. (Yeremia 50:38; 51:9, 12, 13) Babuloni Mkubwa pia hutegemea “maji mengi” yampe himaya na kumtajirisha. Maji haya ya ufananisho ni “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi,” yaani, maelfu ya mamilioni yote ya binadamu ambao juu yao yeye ametawala na ambao kutoka kwao yeye amechota msaada wa vitu vya kimwili. Lakini maji haya ya ufananisho yanakauka pia, au kuondoa msaada.—Ufunuo 17:15, NW; linga Zaburi 18:4; Isaya 8:7.
11. (a) Jinsi gani Babuloni wa kale ‘alifanya dunia yote ilewe’? (b) Babuloni Mkubwa ‘amefanyaje dunia yote ilewe’?
11 Na zaidi, Babuloni wa kale alielezwa kuwa “kikombe cha dhahabu katika mkono wa Yehova, akifanya dunia yote ilewe.” (Yeremia 51:7, NW) Babuloni wa kale alilazimisha mataifa jirani kumeza maonyesho ya kasirani ya Yehova alipoyashinda kijeshi, kuyafanya dhaifu kama wanadamu waliolewa. Katika njia hiyo, alikuwa chombo cha Yehova. Babuloni Mkubwa, pia, amefanya ushindi mwingi kwa kadiri ya kuwa milki ya ulimwenguni pote. Lakini yeye kwa uhakika si chombo cha Yehova. Badala ya hivyo, yeye ametumikia “wafalme wa dunia” ambao pamoja nao yeye hufanya uasherati wa kidini. Yeye hufurahisha wafalme hawa kwa kutumia mafundisho yake ya uwongo na mazoea yenye kutumikisha ili kuweka matungamo ya watu, “wale wanaoikaa dunia,” kuwa dhaifu kama wanadamu waliolewa, wakitii watawala wao bila kuwa na la kufanya.
12. (a) Kisehemu kimoja cha Babuloni Mkubwa katika Japani kilikuwaje na daraka la kumwagwa kwa damu nyingi wakati wa Vita ya Ulimwengu 2? (b) Jinsi gani “maji” yenye kuunga mkono Babuloni Mkubwa yaliondolewa katika Japani, na kukiwa na tokeo gani?
12 Japani ya Shinto hutoa kielelezo kinachostahili kuangaliwa cha jambo hili. Askari-jeshi Wajapani waliiona kuwa heshima ya juu zaidi sana kutoa uhai wao kwa ajili ya maliki—mungu mkuu wa Shinto. Wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, askari-jeshi Wajapani wapatao 1,500,000 walikufa vitani; karibu kila mtu aliona kusalimu amri kuwa utovu wa heshima. Lakini likiwa tokeo la ushinde wa Japani, Maliki Hirohito alilazimika kukana dai lake la uungu. Hilo lilitokeza mwondoleo mkubwa wa “maji” yaliyounga mkono kisehemu cha Shinto cha Babuloni Mkubwa—loo! baada ya Ushinto kuidhinisha umwagaji wa ndoo nyingi za damu katika uwanja wa vita wa Pasifiki! Mdhoofisho huu wa uvutano wa Shinto ulifungua pia njia katika miaka ya juzi kwa ajili ya Wajapani 200,000, ambao walio wengi wao walikuwa hapo kwanza Washinto na Wabuddha, wawe wahudumu walio wakfu na waliobatizwa wa Yehova Bwana Mwenye Enzi Kuu.
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
a Akionyesha chanzo kisicho cha Kikristo cha mengi ya mafundisho, sherehe, na mazoea ya Jumuiya ya Wakristo iliyoasi imani, John Henry Newman kardinali Mkatoliki wa karne ya 19 aliandika hivi katika kichapo chake Essay on the Development of Christian Doctrine: “Utumizi wa mahekalu, na hayo yakiwa yamewekwa wakfu kwa watakatifu fulani, na pindi nyingine yakiwa yametiwa madoido ya matawi ya miti; uvumba, mataa, na mishumaa; matoleo ya kushuhudia wakfu baada ya kupata nafuu ya ugonjwa; maji matakatifu; nyumba za kutunzia mayatima na wenye shida; sikukuu na misimu, tumizi la kalenda, miandamano, kubarikia mashamba; mavazi ya makasisi, kipara utosini, pete katika ndoa, kugeukia Mashariki, mifano kwenye tarehe ya baadaye, labda wimbo wa kieklesia, na Kyrie Eleison [wimbo “Bwana, Urehemu”], chanzo cha yote ni upagani, yakatakaswa kwa kukubaliwa ndani ya Kanisa.”
Badala ya kutakasa ibada ya sanamu kama hiyo, “Yehova Mweza Yote” huonya Wakristo “Ondokeni kutoka miongoni mwao, na kujitenga nyinyi wenyewe, . . . na acheni kabisa kugusa kitu kisicho safi.”—2 Wakorintho 6:14-18, NW.
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 237]
Churchill Afichua ‘Ukahaba’
Katika kitabu chake The Gathering Storm (1948), Winston Churchill huripoti kwamba Hitla alimweka rasmi Franz von Papen kuwa waziri wa Ujeremani kwenye Vienna ili “kudhoofisha au kuvuta watu mashuhuri katika siasa za Austria.” Churchill hunukuu waziri wa U.S. katika Vienna kuwa akisema hivi juu ya von Papen: “Kwa jinsi ya ujasiri zaidi sana na ya kudharau zaidi sana . . . Papen aliendelea kuniambia kwamba . . . yeye alikusudia kutumia sifa yake akiwa Mkatoliki mwema apate uvutano pamoja na Waaustria kama Kardinali Innitzer.”
Baada ya Austria kukubali ushinde na vikosi vya Hitla vyenye kushambulia ghafula vikiwa vimepiga gwaride kuingia Vienna, Innitzer kardinali Mkatoliki aliamuru kwamba makanisa yote ya Austria yapandishe bendera ya swastika, yapige kengele zayo, na yatoe sala kwa ajili ya Adolf Hitla kwa heshima ya ukumbusho wa siku ya kuzaliwa kwake.
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 238]
Chini ya kichwa hiki, makala inayofuata ilitokea katika chapa ya kwanza ya The New York Times ya Desemba 7, 1941:
‘SALA YA VITA’ KWA AJILI YA REICH
Maaskofu wa Kikatoliki katika Fulda Waomba Baraka na Ushindi
Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujeremani lililokusanyika katika Fulda limependekeza ianzishwe ‘sala ya vita’ maalumu ambayo itasomwa mwanzoni na mwishoni mwa ibada zote za kimungu. Sala hiyo husihi Mungu abariki silaha za Ujeremani kwa ushindi na kutoa himaya kwa maisha na afya ya askari-jeshi wote. Maaskofu hao waliwaagiza zaidi makasisi wa Kikatoliki waweke na kukumbuka katika mahubiri maalumu ya Jumapili angalau mara moja kwa mwezi askari-jeshi Wajeremani ‘barani, baharini na hewani.’”
Makala hii iliondolewa kwenye chapa za baadaye za nyusipepa hiyo. Desemba 7, 1941, ndiyo siku Japani, nchi fungamani na Ujeremani, iliposhambulia meli za U.S. kwenye Pearl Harbor.
[Picha katika ukurasa wa 244]
-