Wimbo Na. 85
Thawabu Kamili Kutoka kwa Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova ni mwaminifu ajua,
Kuna nyakati ambazo,
Watumishi wake hupata shida,
Ilitabiriwa kale.
Ikiwa umeacha familia,
Makao au rafiki,
Utapata ndugu na dada sasa,
Na uzima wa milele.
(KORASI)
Yehova Mungu akukumbuke
Upate thawabu toka kwake.
Kimbilio upate kwake.
Yehova kwa kweli; ni mwaminifu.
2. Iwe ni kupenda ama ni hali;
Wengine hawana wenzi.
Wanapoutanguliza Ufalme,
Na kutumikia Mungu.
Wanaoupa useja nafasi,
Tunajua ni wapweke.
Tuwe kama ndugu na dada kwao,
Nasi tuwatie moyo.
(KORASI)
Yehova Mungu akukumbuke
Upate thawabu toka kwake.
Kimbilio upate kwake.
Yehova kwa kweli; ni mwaminifu.
(Ona pia Amu. 11:38-40; Rut. 2:12; Mt. 19:12.)