Wimbo Na. 2
Asante, Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Asante Mungu wetu kwa sababu,
Umetupa nuru ya ajabu.
Asante kwa pendeleo la sala,
Twaweza kukujia na shida.
2. Asante, Yehova, kwa Mwana wako,
Aliyeushinda ulimwengu.
Asante kwa kutupa maagizo.
Hivyo twaepuka matatizo.
3. Asante Yehova kwa pendeleo,
La kukutangaza wewe leo.
Asante ole zote zitakwisha,
Baraka zako zaburudisha.
(Ona pia Zab. 50:14; 95:2; 147:7; Kol. 3:15.)