Wimbo Na. 124
Wakaribisheni
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova huonyesha ukarimu.
Ubaguzi hana, si mudhalimu.
Jua nayo mvua,
hanyimi yeyote.
Hutoa chakula kwa wote.
Tuwafadhilipo watu wa chini,
Twamwiga Yehova, anathamini.
Naye Baba yetu, atatufadhili,
Kwa wema wetu na fadhili.
2. Hatuwezi kujua matokeo,
Ya kutokuwa na upendeleo.
Hata iwe kwamba,
hatuwafahamu,
Twawakaribisha kwa hamu.
Nasi twawaambia, ‘karibuni!’
Wajistareheshe bila huzuni.
Mungu awajua wote wamwigao.
Wawafadhilio wenzao.
(Ona pia Mdo. 16:14, 15; Rom. 12:13; 1 Tim. 3:2; Ebr. 13:2; 1 Pet. 4:9.)