Wimbo Na. 79
Nguvu za Fadhili
Makala Iliyochapishwa
1. Twashukuru kumujua Mungu,
Neno lake pia.
Ni Mungu mwenye hekima nyingi,
Ana upendo, fadhili.
2. Kristo anawaalika wote,
Awapumuzishe.
Waichukue nira laini,
Wapate kuburudishwa.
3. Yehova na Yesu Bwana wetu,
Tuwaige wao.
Katika yote tunayofanya,
Na tuonyeshe fadhili.
(Ona pia Mika 6:8; Mt. 11:28-30; Kol. 3:12; 1 Pet. 2:3.)