WIMBO NA. 81
Maisha ya Painia
Makala Iliyochapishwa
1. Jua lachomoza, kunapambazuka.
Macho ni mazito,
Twasali kisha twaondoka
Tabasamu nyingi, wanasikiliza.
Hata wasiposikiliza,
Hatuchoki kamwe.
(KORASI)
Ni maisha yetu;
Tumeyachagua.
Kufanya mapenzi ya Mungu
Tutavumilia,
Kuwe mvua, jua.
Kwa kuwa twampenda sana Yehova.
2. Mwishoni mwa siku, jua linatua.
Japo tumechoka
Moyoni tunayo furaha.
Ni maisha yetu, ya kujidhabihu.
Yehova twashukuru,
Kwa baraka zako nyingi.
(KORASI)
Ni maisha yetu;
Tumeyachagua.
Kufanya mapenzi ya Mungu
Tutavumilia,
Kuwe mvua, jua.
Kwa kuwa twampenda sana Yehova.
(Ona pia Yos. 24:15; Zab. 92:2; Rom. 14:8.)