Wimbo 208
Wimbo wa Kushangilia
1. Panda zalia. Furaha nyingi.
Mwana wa Mungu atawala.
Patu zalia. ’Vazi yameta.
Sauti hii yasikiwa:
(Korasi)
2. Kwa kuhubiri na kufundisha,
Wengi wavutwa kwa Yehova.
Nao waimba Nyimbo za shangwe,
Kote kote, wazivumisha!
(Korasi)
3. Tuendelee Kuhurumia
Watu wa Mungu, ndugu zetu.
Kuimba kwetu kulete sifa
Kwa Yehova, kwani ni mwema.
(KORASI)
Siku ya Yehova. (Ni shangwe.)
Ufalme kudumu (Shangwe.)
Viumbe wote na (’Furahi.)
Sifuni Mungu na mwimbe:
“Yehova Mungu, wokovu wetu
Pia Yesu Mufalme wetu.”