Wimbo 133
Kupanda Mbegu za Ufalme
1. Njoni, watumwa wote wa Yehova,
Muliojitoa kwake.
Fanyeni kazi aliyowapa na
Bwana wenu fuateni.
Mbegu za ukweli zienezeni
Pale palipo rutuba
Sifa kwa Mungu, mukifanya kazi
Kutimiza fungu shambani.
2. Kwenye njia mbegu zikianguka,
“Ndege” wa Shetani wala;
Udongo wa mwamba zikiendea,
Joto linazimaliza.
Wasiwasi, pupa husonga mbegu
Kabla hazijakomaa.
Lakini, nyingine zitaanguka
Katika udongo muzuri.
3. Wingi wa mbegu palipo rutuba
Wawategemea sana.
Kwa saburi, pendo, fukuza ndege,
Uyapunguze mateso.
Kwa kuwa macho ondoa miiba,
Midogo hata mikubwa.
Tumaini ni kuvuna kwa shangwe
Thelathini na hata mia.