Wimbo 93
Mahali pa Ibada Penye Kupendeza pa Yehova
1. Ni zuri hekalu lako,
Na nyua za watu wako!
Natamani nizijie,
Niimbe zaidi humo
Niimbe zaidi humo.
2. Yehova, tukujiapo,
Utupe nguvu nyingine,
Pendo, kweli, tunalishwa
Tutumike kwa ujana,
Tutumike kwa ujana.
3. Siku ni bora nyuani,
Elfu kwingine ni duni.
Afadhali tuwe kwako
Kuliko nao waovu,
Kuliko nao waovu.
4. Kwa Yah nuru, ngao, viko
Kwa wazaao matunda.
Chema chote kilichoko
Awapa zizini mwake,
Awapa zizini mwake.