Wimbo 121
Ukweli Unaoweka Watu Huru
1. Torati ya Musa na unabii wa kale
Ulikuwa kivuli cha ukweli wa leo.
Ukweli unaoweka huru wa Uzao
—Jinsi kwa Yesu twaweza kupata uzima.
2. Mimi Yesu ni ‘njia, ukweli na uzima.’
Kwa damu yake alichukua dhambi zetu,
Atetee jina la Babaye ni wa kweli.
Na kushinda maadui wa Yehova sasa.
3. Kwa Mwana wa Yehova Yesu, kuna ukweli.
Kuna uhakika dhambi zote zitakwisha.
Yeye ni Uzao atukuzaye Yehova.
Nasi twatangaza ni Kuhani na Mufalme.
4. Tunahubiri juu ya Yesu kwa ukweli.
Tu tayari kuhubiri; na tuna amani.
Ufalme wa Masihi na tuutegemeze.
Tuukweze nafusi yote, wote waone.