Wimbo 43
Haya Mbele, Enyi Wahudumu wa Ufalme!
1. Songeni hubiri Ufalme
Kwao watu kila nchi.
Mioyo kupenda jirani,
Saidia wapole.
Kuutukuza utumishi
Tuone tunavyovaa.
Huduma yetu ya thamani;
Tutabariki Yehova.
(Korasi)
2. Wahudumu wapya songeni
Tazamieni tuzo.
Sahauni muliyoacha,
Neno ’liwape nguvu.
Na mukiwa wajumbe safi
Epukeni ulimwengu.
Yafaa wahudumu Mungu
Waache ya ulimwengu.
(Korasi)
3. Na tusonge wote pamoja,
Mabaki na “kondoo.”
Wazee, vijana na wake,
Mwambatane na kweli.
Tuna huduma takatifu
Tuiheshimu zaidi.
Wapenda kweli, ni faraja
Na heshima kwake Mungu.
(KORASI)
Songa mbele,
Hubiri Ufalme huku na huku.
Songa mbele,
Iweni upande wake Yehova.