Wimbo 28
Bariki Kukutana Pamoja Kwetu
1. O Yehova tubariki,
Tunapokutanika.
Asante kwa mikutano;
Roho ikae nasi
2. Uhitaji wa kiroho;
Jaza kwa Neno lako.
Funza akili na ndimi,
Jaza mioyo pendo.
3. Twakutana kuabudu;
Tuwe watakatifu.
Tukujue vema sana
Tudumishe upole.
4. E Baba, utubariki;
Kwa umoja, amani.
Twataka kutumikia,
Tukuze Enzi yako.