Wageuze Watu Waliache Giza Waingie Nuruni
1 Giza la kiroho lafunika dunia. (Isa. 60:2) Tangu mwanadamu aanguke katika dhambi, Shetani, “mungu wa huu mfumo wa mambo,” ameweka watu katika giza la kiroho, na tokeo limekuwa hali mbaya sana ya maadili.—2 Kor. 4:4, NW.
2 Sasa kwa kuwa sisi tumekwisha kupewa nuru kwa kweli, je, sisi husikitikia watu kama Yesu alivyofanya? (Mt. 9:36) Ikiwa ndivyo, sisi tutathamini umaana wa utume aliompa mtume Paulo wa ‘kufumbua macho ya watu na kuwageuza waliache giza na kuingia nuruni waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu.’—Mdo. 26:16-18.
TIA NURU KATIKA AKILI NA MIOYO
3 Kwa kuwa Shetani hupofusha akili na kufisha ganzi mioyo ya mateka wake, twaweza kuwasaidiaje? Twahitaji kufikia akili na mioyo yao kwa Neno la Mungu. Paulo alisali kwamba macho ya mioyo ya Waefeso itiwe nuru. (Efe. 1:17, 18) Hakuna kitu kilicho na nguvu nyingi kuliko Neno la Mungu katika kufikia mioyo. (Ebr. 4:12) Kujua hivyo kwapasa kutusukuma tusitawishe ustadi katika kutumia Biblia tunenapo na wengine.
4 Majibu yako kwa maswali yafuatayo huenda yakakusaidia kuwa stadi zaidi katika huduma. Je! wewe hujitayarisha vizuri kwa ajili ya utumishi wa shambani? Je! wewe huwa na pindi za mazoezi ujifahamishe vifungua mazungumzo ambavyo hunasa kupendezwa kwa mwenye nyumba? Je! wewe hujitahidi kujifunza Kichwa cha Mazungmzo cha wakati uliopo na kujaribu kukitumia? Je! wewe hujaribu kutoa sababu zenye kushawishi kwa Maandiko milangoni?—Mdo. 17:2.
MNARA WA MLINZI NI MSAADA
5 Mnara wa Mlinzi limesaidia mamilioni ya watu waliache giza waingie nuruni. Linatuonyesha jinsi ya kutumia kanuni za maadili za Biblia, tuelewe unabii wayo mbalimbali kwa siku zetu, na kutofautisha kati ya dini ya kweli na dini bandia ili kutembea katika njia anayoikubali Yehova.
6 Ukweli wa Biblia kama unavyotetewa na Mnara wa Mlinzi umetokeza nini? Watu wa kila aina wanasaidiwa waelekee wokovu kupitia maarifa sahihi juu ya Mungu na Mwana wake. (Yn. 17:3; 1 Tim. 2:4) Msomaji mmoja aliandika hivi: ‘Jinsi ninavyothamini Mnara wa Mlinzi! Makala zapasa kusaidia wote waone waziwazi nyakati na majira tunamoishi. Asanteni sana kwa kiasi cha utafiti, uchunguzi, na kazi mnayofanya ili kutayarisha Mnara wa Mlinzi, ambalo kwa kweli ni chakula cha kiroho.’
TUMIA UTAMBUZI
7 Wakati wa huu mwezi wa pili wa kampeni ya uandikishaji wa Mnara wa Mlinzi, tunahitaji kutafuta fursa za kuwageuza watu waliache giza waingie nuruni. Mazungumzo ya Biblia tunayokuwa nayo pamoja na watu tunaotembelea nyumba kwa nyumba hutusaidia kufanya hivyo. Wakati tunapopata watu ambao huonyesha kupendezwa halisi na ujumbe wa Ufalme, twaweza kutaja manufaa ya kusoma Mnara wa Mlinzi kwa ukawaida. Toa uandikisho wa mwaka mmoja au wa miezi sita ikifaa. Kwa sababu ya mabadiliko ya gharama za posta tafadhali usikubali maandikisho ya mwaka kwa miaka mingi. Hakikisha umerudi kwa ajili ya ahadi zozote zinazofanywa za uandikisho.
8 Tuendapo nyumba kwa nyumba, tutoapo ushuhuda wa barabarani, au kutoa ushuhuda vivi hivi kwa wafanyakazi wenzetu, wanashule wenzetu, na watu wa jamaa, twashiriki kweli ambayo huwaweka watu huru. (Yn. 8:32) Mnara wa Mlinzi ni kifaa cha pekee ambacho chaweza kuwasaidia wapate uhuru na kupata utimizo wa tumaini la uhai wa milele, likigeuza waliache giza na kuingia nuruni.