Wimbo 25
Vitu Vyema vya Mungu
1. Mungu alifanya
Vitu vyote vyema.
Kula, kunywa, kazi,
Ni zawadi bora.
Na pia tamaa
Kuishi milele.
Tunatumaini
Kwa sababu hiyo.
2. Mapenzi yake Yah
Kubariki watu
Wamupende sana
Zaidi zaidi.
Kwa zawadi zake
Watu watumie;
Milele milele
Atakuwa nao.
3. Kazi bora sana
Ya habari njema
Tuikamilishe;
Kwa bidii nyingi.
Hiyo ni zawadi
Inafurahisha.
Ni kazi njema we
Tuliyoagizwa.
4. Kwa hekima sote
Tutende daima
Kusudi la Mungu
Na tulitangaze.
Pendeleo hili
Na tulithamini.
Twatimiza hayo
Tupendeze Mungu.